Pata taarifa kuu
Gabon

Waasi wa Seleka nchini Jamuhuri ya Afrika ya kati wawasili Gabon

Viongozi wa kundi la waasi wanaoshikilia miji muhimu nchini Jamuhuri ya Afrika ya Kati waliwasili hapo jana mjini Libreville huko Gabon kwa ajili ya kufanya mazungumzo na Serikali ili kumaliza mzozo nchini mwao.

Rais wa Jamuhuri ya Afrika ya Kati, Froncois Bozize
Rais wa Jamuhuri ya Afrika ya Kati, Froncois Bozize AFP PHOTO/JOHN THYS
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Afrika ya kati, Froncois Bozize pia alisafiri hiyo jana kuelekea Gabon kukutana na Rais wa Taifa hilo Denis Sassou Nguesso ambaye ndiye mpatanishi wa mgogoro kati ya pande mbili zinasohasimiana nchini Jamuhuri ya Afrika ya Kati, ambapo mazungumzo ya kuleta amani yanatarajiwa kuanza baadae juma hili.

Waasi wa Seleka mwishoni mwa juma walirejea madai yao kuwa makubaliano yoyote ya kuleta amani yanayotarajiwa kuanza hapo kesho lazima yaambatane na kuondoka madarakani kwa Rais wa Taifa hilo, Froncois Bozize.

Jumuia ya Nchi za Afrika ya kati CEEAC ina matumaini kuwa itaratibu mazungumzo hayo kati ya waasi na Rais Bozize jijini Libreville nchini Gabon ili kuweza kumaliza mzozo nchini Jamuhuri ya Afrika ya Kati.

Hata hivyo wasiwasi uliopo ni kuwa mazungumzo hayo huenda yakaingia dosari kuwa kuwa Waasi wamekuwa wakisisitiza kuwa Rais Bozize aliyeingia madarakani mwaka 2003 ni lazima ajiuzulu shinikizo ambalo Bozize hakubaliani nalo.

Katika mazungumzo hayo, Ujumbe wa Serikali ya Rais Bozize utatoa mapendekezo juu ya mabadiliko ndani ya jeshi, mipango ya maendeleo ya kiuchumi na Tratibu za uchaguzi.

 

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.