Pata taarifa kuu
JAMHURI YA AFRIKA YA KATI

Mazungumzo ya amani nchini Afrika ya Kati kuanza Jumanne nchini Gabon

Serikali ya Jamhuri ya Africa ya Kati na muungano wa waasi, wanajiandaa kwa mazungumzo ya amani yaliyopangwa kuanza nchini Gabon siku ya Jumanne ambapo ujumbe wa kwanza uko mbioni kuwasili katika mji mkuu Libreville. 

Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Francois Bozize
Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Francois Bozize AFP PHOTO/ SIA KAMBOU
Matangazo ya kibiashara

Jumuiya ya kiuchumi ya nchi za Afrika ya Kati inataraji kuwa mwenyeji wa mazungumzo hayo kati ya waasi na Rais Francois Bozize , mazungumzo ambayo pia yanaungwa mkono na Marekani na Baraza la Usalama la umoja wa mataifa.

Hapo jana Waasi walifanikiwa kuteka miji miwili zaidi usiku wa kuamkia Jumamosi, waziri wa utawala wa majimbo Yoshua Binoua amethibitisha.

Binoua amesema kuwa waasi hao wameteka miji hiyo iliyoko karibu na mji wa Bambari mji ambao tayari upo chini ya udhibiti wa waasi wa Seleka jambo linaloashiria nia yao ya kufanya vita hata wakati wa majadiliano ya amani.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.