Pata taarifa kuu
Mali

Waziri Mkuu wa Mali aanza kuunda serikali ya Umoja wa Kitaifa

Waziri Mkuu mpya  wa Mali Diango Cissoko ameanza kuunda serikali ya Umoja wa Kitaifa akisema lengo la kubwa ni  kumaliza mzozo kati ya serikali ya Bamako na makundi ya wapiganaji Kaskazini mwa nchi hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Cissoko ambaye anachukua nafasi ya Waziri Mkuu wa zamani Cheick Modibo Diarra aliyeshurutishwa kujiuzulu mapema Juma hili, ameahidi kuhakikisha kuwa anarejesha utulivu Kaskazini mwa nchi hiyo.

Waziri Mkuu mpya hajagusia kuhusishwa kwa jeshi la kimataifa kusaidia kupambana na makundi hayo ya wapiganaji, huku wachambuzi wa mambo wakisema kuwa Waziri Mkuu wa zamani Diarra alioneka kuwa kikwazo kwa mpango wa jeshi la mataifa ya Afrika Magharibi kupambana  na wapiganaji hao.

Umoja wa Ulaya na Marekani zimesifu hatua za serikali ya Mali kumteua haraka Waziri Mkuu mpya ambaye anasema ni mtu ambaye anaheshimiwa na kufahamika  kimataifa na uhusiano wake na mataifa ya kigeni utakuwa mzuri.

Hata hivyo, mataifa ya Magharibi yameshtumu namna Diarra alivyoshurutishwa kujiuzulu na jeshi nchini humo chini ya Kapteni Amadou Sanogo aliyeongoza mapinduzi dhidi ya serikali mapema mwa huu.

Aidha, mataifa hayo yamelitaka jeshi nchini humo kuachana na siasa na badala yake kulinda maisha ya raia nchini humo.

Jeshi nchini humo linasema halifurahishwa na namna viongozi wa mataifa ya Afrika Magharibi wanavyopanga kukabiliana na makundi ya wapiganaji Kaskazini mwa nchi hiyo kutumia majeshi ya ECOWAS kwa kile wanachosema kuwa wao pia wana uwezo wa kupigana nao ikiwa watawezeshwa kwa kupewa fedha na silaha.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.