Pata taarifa kuu
AU

Umoja wa Afrika washtumu hatua ya kulazimishwa kujiuzulu kwa Waziri Mkuu wa Mali

Umoja wa Afrika umeshtumu hatua ya kulazimishwa kwa Waziri Mkuu wa Mali Cheick Modibo Diarra kujiuzulu na kutaka jeshi kutii uongozi wa kiraia nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

AU imesisitiza kuwa ni sharti jeshi nchini humo kuachana kabisa na kuhitilafiana na uongozi nchini humo shutuma ambazo pia zimetolewa na Umoja wa Mataifa pamoja na Marekani.

Waziri Mkuu mpya  Diango Cissoko amesema lengo lake kuu ni kuchukua uthibti wa eneo la Kaskazini mwa nchi hiyo kutoka kwa makundi ya wapiganaji waliochukua uthibiti wa eneo hilo mapema mwaka huu.

Diarra alikamatwa siku ya Jumatatu nyumbani kwake jijini Bamako baada ya agizo kutoka kwa kiongozi wa kijeshi aliyeongoza mapinduzi hayo ya kijeshi Amadou Sanogo na kulazimishwa kujizulu pamoja na familia yake.

Diarra aliteuliwa mwezi Aprili baada ya jeshi kukabidhi madaraka kwa umma ili kuundwa kwa serikali ya mpito baada ya shinikizo kutoka kwa Jumuiya ya Kimataifa na Umoja wa Afrika.

Katika siku za hivi karibuni kumekuwa na hali ya wasiwasi kati ya wanajeshi wanaomuunga mkono Diarra na wale waliopindua serikali ya Mali chini ya kiongozi wao Sanogo.

Wakati wa uongozi wake kama Waziri Mkuu, Diarra alikuwa tayari na viongozi wengine wa matafa ya Arika Magharibi kutuma majeshi ya ECOWAS Kaskazini mwa Mali kukabiliana na makudi ya waasi yanayotawala eneo hilo.

Idadi kubwa ya wanajeshi wa  Mali wanapinga wazo la kepelekwa kwa wanajeshi wa Kimataifa Kaskazini mwa nchi hiyo kwa kile wanachokisema kuwa wao wanaweza kupambana na makundi hayo  ikiwa watapata msaada wa kifedha.
 
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.