Pata taarifa kuu
MALI-MAREKANI

Waziri mkuu wa Mali autaka Umoja wa Mataifa kuidhinisha kupelekwa kwa vikosi vya kigeni nchini mwake

Waziri mkuu wa Mali Cheick Modibo Diarra ameuomba Umoja wa Mataifa kuruhusu kupelekwa kwa vikosi vya Umoja huo nchini mwake kukabiliana na waasi ambao wanashikilia maeneo ya kaskazini mwa nchi hiyo.

Waziri mkuu wa Mali, Cheick Modibo Diarra wakati akihutubia kikao cha Baraza la Usalama
Waziri mkuu wa Mali, Cheick Modibo Diarra wakati akihutubia kikao cha Baraza la Usalama UN Photo/Marco Castro
Matangazo ya kibiashara

Kauli ya waziri huyo inakuja wakati ambapo rais wa Ufaransa, Francois Hollande akihutubia kikao cha Baraza la Usalama ametaka Umoja huo kuhalalisha kupelekwa kwa vikosi vya kijeshi toka Muungano wa ECOWAS kusaidia kutwaa maeneo ya kaskazini mwa nchi hiyo.

Waziri mkuu Diarra amewaambia wajumbe wa mkutano wa mwaka wa Umoja wa Mataifa kuwa nchi yake inahitaji msaada wa haraka wa majeshi ya kigeni kwenda nchini humo kukabiliana na waasi walioteka maeneo ya kaskazini.

Wachambuzi wa masuala ya siasa wanasema kuwa kauli ya waziri mkuu Diarra ilitarajiwa kwakuwa mara kadhaa amesikika akitaka usaidizi wa vikosi vya kigeni huku akipata upinzani toka kwa wanajeshi wa ndani ambao wanadai wanauwezo wa kukabiliana na waasi hao.

Muungano wa nchi za magharibi mwa Afrika ECOWAS ulitangaza kuidhinisha kikosi cha wanajeshi kupelekwa nchini Mali lakini walihitaji baraka kutoka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuidhinisha operesheni hiyo.

Lakini wakati Ufaransa ikunga mkono hatua ya kupelekwa kwa vikosi vya kigeni, waziri wa mambo ya nje wa Marekani Hillary Clinton ameonya dhidi ya kuchukua hatua hizo akitaka kwanza kurejeshwa kwa serikali ya kidemokrasia nchini humo na sio ya mpito.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.