Pata taarifa kuu
Guinea Bissau-Cote D' Ivoire

Vikosi vya Guinea Bissau kurejea kambini, Rais Ouatara amfukuza kazi waziri kwa rushwa

Vikosi vya Guinea Bissau vimeapa hii leo kurejea katika kambi zao baada ya Mamlaka ya mpito kuunda Serikali mpya iliyohusisha afisa wa kijeshi aliyeshiriki mapinduzi ya Aprili 12 nchini humo.

ALFA BA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Mpito wa Guinea Bissau, Serifo Nhanadjo alitia saini makubaliano ya kuunda baraza lenye mawaziri 27 chini ya waziri mkuu Rui Duarte Barros, akiwemo waziri wa ulinzi Kanali Celestino Carvalho, mmoja wanajeshi waliomuondoa Rais wa nchi hiyo madarkani.

Msemaji wa majeshi yaliiongoza mapinduzi, kanali Daba Na Walna ameliambia shirika la habari la ufaransa kuwa hivi sasa watarejea kambini kwa kuwa Serikali ya mpito imepatikana.

Siku ya jumamosi majeshi, Bunge na vyama vya kisiasa vilitia saini makubaliano ya kutafuta namna ya kumaliza vurumai zilizosababishwa na mapinduzi.

Miongoni mwa makubaliano hayo ni pamoja na uundwaji wa tume ya uchaguzi,ambapo itaongozwa na jaji ambaye atazipitia tena sheria za uchaguzi.

Wakati huohuo Rais wa Cote D ivoire, Allasane Ouatara amemfuta kazi waziri wa masuala ya Uhusiano wa Afika Adama Bictogo akishutumiwa kujihusisha na vitndo vya Rushwa.

Ofisi ya Rais imesema Ouattara amemfuta kazi rasmi Bictogo aliyekuwa akihudumu kwenye serikali yake.

Kwa mujibu wa gazeti la Jeune Afrique la nchini Cote d ivoire, Bictogo kwa kufanya dhuluma ya malipo ya watu walioathirika na sumu iliyomwagwa Baharini na Meli ya mizigo jijini Abidjan

Bictogo pia, alikuwa miongoni mwa wajumbe wa ECOWAS walio na kibarua cha kutatua mzozo wa kisiasa nchini Mali.

 

 

 

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.