Pata taarifa kuu
SENEGAL-MALI-GUINEA-BISSAU

ECOWAS kushusha vikwazo kwa Tawala za Kijeshi zilizofanya Mapinduzi katika nchi za Mali na Guinea-Bissau

Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi ECOWAS imeongeza kitisho cha kushusha vikwazo kwa Viongozi wa Mali na Guinea-Bissau ambao wametekeleza mapinduzi na kusitisha kurejesha madaraka kamili kwa tawala za mpito za kiraia zenye mamlaka ya kuitisha uchaguzi.

Rais wa Cote D'Ivoire na Rais wa ECOWAS Alassane Ouattara akihutubia Marais wa Jumuiya hiyo juu ya hali ya Mali na Guinea-Bissau
Rais wa Cote D'Ivoire na Rais wa ECOWAS Alassane Ouattara akihutubia Marais wa Jumuiya hiyo juu ya hali ya Mali na Guinea-Bissau Reuters/Thierry Gouegnon
Matangazo ya kibiashara

Kauli ya ECOWAS imetolewa na Marais wa Jumuiya hiyo ambao walikutana nchini Senegal kujadili hatima ya nchi za Mali na Guinea-Bissau ambazo zimeshuhudiwa wanajeshi wakitekeleza mapinduzi yasiyomwaga damu dhidi ya tawala halali zilizochaguliwa na raia.

Viongozi wa Nchi wanachama wa ECOWAS wameshinikiza Utawala wa Kijeshi wa Guinea-Bissau kuwaaachia wafungwa waote wa kisiasa ambao wanawashikilia tangu walipofanikisha mapinduzi yao mwezi uliopita.

Marais ambao walikutana nchini Senegal licha ya kutishia kuweka vikwazo kwa nchi hizo za Mali na Guinea-Bissau iwapo zikishindwa kutekeleza maagizo yao lakini wamepongeza kitendo cha kuachiwa kwa Waziri Mkuu wa zamani wa Guinea-Bissau Carlos Gomes pamoja na Kaimu Rais Raimundo Pereira.

Kitisho hiki cha ECOWAS kuweka vikwazo kinakuja siku moja baada ya Umoja wa Ulaya EU kushusha rungu la vikwazo kwa Utawala wa Kijeshi wa Guinea-Bissau ambao umeshindwa kuheshimu serikali ya kiraia iliyokuwa inaongoza.

Vikwazo vya ECOWAS kwa Utawala wa Kijeshi unalenga masuala ya uchumi pamoja na kusafiri huku wakiitaka Guinea-Bissau kumuapisha Spika wa Bunge awe Rais ili aongoze serikali ya mpito itakaitisha uchaguzi mapema.

Rais wa Jumuiya hiyo ambaye anaongoza nchi ya Cote D'Ivoire Alassane Ouattara alifungua kikao chao kwa kusema hawawezi kuwavumulia viongozi wa kijeshi ambao wanashindwa kutekeleza makubaliano waliyoyasimamia.

ECOWAS imeamuru kupelekwa kwa Vikosi vyake vya Jeshi katika nchi za Mali na Guinea-Bissau ili kukabiliana na vitendo vya mapinduzi ambavyo vimekuwa vikipangwa na baadhi ya wanajeshi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.