Pata taarifa kuu
GUINEA-BISSAU

ECOWAS kuiwekea vikwazo Guinea-Bissau wakati huu Kikosi cha kwanza cha wanajeshi kikiwasili

Jumuiya ya Kujihami ya Nchi za Afrika Magharibi ECOWAS imetangaza kuwa katika hatua za mwisho kuiwekea vikwazo nchi ya Guinea-Bissau ambayo inaongozwa na utawala wa kijeshi uliofanya mapinduzi yasiyo ya kumwaga damu wakati huu kikosi cha askari wake wakitarajiwa kuwasili Banjul.

Wanajeshi wa Guinea-Bissau ambao wamefanikisha mapinduzi ya kijeshi
Wanajeshi wa Guinea-Bissau ambao wamefanikisha mapinduzi ya kijeshi Reuters
Matangazo ya kibiashara

Uamuzi wa ECOWAS kutaka kuiwekea vikwazo serikali ya kijeshi inayoongozwa na Jenerali Antonio Indjai imekuja kutokana na utawala huo kutokuwa tayari kufanya mazungumzo ya kuangalia namna ya kurejesha serikali ya kiraia waliyoipindua tarehe 12 ya mwezi April mwaka huu.

Taarifa ambayo imetolewa na ECOWAS imetoa onyo itashusha vikwazo kwa serikali ya Guinea-Bissau katika Mkutano wake ujao iwapo serikali ya Kijeshi ya nchi hiyo itashindwa kurejesha serikali ya kiraia.

ECOWAS wametishia kuiwekea vikwazo Guinea-Bissau baada ya mazungumzo yaliyodumu kwa saa kumi na mbili kushindwa kutoa matunda kutokana na serikali ya kijeshi kukataa kutekeleza mapendekeo ya nchi wanachama kurejesha serikali ya kiraia.

Taarifa hiyo imesema kitendo cha kushindwa kufikia muafaka kwa mazungumzo ya kurejesha utawala wa kiraia kuna maana wakati wowote vikwazo dhidi ya Guinea-Bissau vitatangazwa ikiwa ni shinikizo la kukubalia mapendekezo ya ECOWAS.

Vikwazo hivyo vimetajwa kuwalenga moja kwa moja Viongozi wa Serikali ya Kijeshi pamoja na biasahara na uchumi wa nchi hiyo ili kuidhibiti isiweze kuwa na nafasi ya kufanya shughuli zake kama ilivyokuwa awali.

Katika hatua nyingine Kikosi cha kwanza cha Wanajeshi kutoka Jumuiya ya Kujihami ya Nchi za Afrika Magharibi ECOWAS kikiwa na wanajeshi kati ya mia tano hadi mia sita kinatarajiwa kuwasili Najul kwa ajili ya kuanza kuchukua hatua za kurejesha serikali ya kiraia.

Wanajeshi hao watakuwa na nafasi ya kuhakikisha serikali ya kijeshi inaondoka madarakani baada ya muda wa saa sabini na mbili walizopewa kutekeleza maazimio ya ECOWAS kukamilika bila ya hatua zozote kuchukuliwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.