Pata taarifa kuu
KENYA

Baadhi ya wanasiasa nchini Kenya wahoji hatua ya serikali kumrejesha Bethuel Kiplagati kwenye tume ya TJRC

Serikali ya Kenya imeingia matatani kutokana na kutuhumiwa kufanya siri ya masuala kadhaa yanayohusiana na ukiukwaji wa Haki za Binadamu yanayostahili kuchunguzwa na Tume ya Ukweli, Haki na Maridhiano inayoongozwa na Bethwel Kiplagat anayekosolewa vikali. 

Bethuel Kiplagat mwenyekiti mpya wa tume ya maridhiano nchini Kenya
Bethuel Kiplagat mwenyekiti mpya wa tume ya maridhiano nchini Kenya Reuters
Matangazo ya kibiashara

Serikali imemrejesha kwenye wadhifa wake Kiplagat ambaye anatuhumiwa kutumika kuficha maovu ya serikali huku akidaiwa kuhusika kwenye mauaji ya halaiki yaliyofanyikaKaskazini mwa Kenya.

William Maranga ni Mchambuzi wa Siasa nchini Kenya ambaye naye anaona kurejeshwa kwenye nafasi yake ya kuongoza Tume ya Ukweli, Haki na Maridhiano ni hatua ya kuendelea kulinda maslahi ya wakubwa.

Uteuzi wa kiongozi huyo umeendelea kuamsha hiia kali kwa baadhi ya wanasiasa na wananchi ambao wanaona kuwa uteuzi wake umekuwa wa kisiasa zaidi kuliko kuzingati maslahi ya wakenya ambao tayari walikuwa wameanza kujenga imani na tume hiyo.

Kiplagat alijiondoa kwenye nafasi ya uenyekiti wa tume hiyo mwaka 2009 kupisha uchunguzi baada ya kutuhumiwa kuhusika kuficha maovu na kuchangia kutokea kwa mauaji ya halaiki ya mwaka 1984 kwenye mji wa Wagalla.

Hata hivyo uteuzi huo umeonekana kuungwa mkono na wabunge wengi wakiamini kuwa huenda sasa tume hiyo ikafanya kazi kama ilivyokusudiwa hapo awali kabla ya kuanza kusuasua.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.