Pata taarifa kuu
GUINEA-BISSAU

Wagombea watano wa urais nchini Guinea-Bissau walaani mapinduzi ya kijeshi

Utawala wa Kijeshi nchini Guinea-Bissau umetangaza kufunga mipaka yake pamoja na kufunga njia za usafiri za anga na baharini wakati huu ambapo katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa UN Ban Ki Moon akilaani kuundwa kwa serikali ya mpito akisema inakuza mgogoro huo. 

Ramani ya nchi ya Guinea-Bissau
Ramani ya nchi ya Guinea-Bissau Reuters
Matangazo ya kibiashara

Katibu Mkuu wa UN Ban amesema kile ambacho kinafanyika nchini Guinea-Bissau kinastaili kuendelea kulaaniwa na kusihi utawala wa kiraia unastahili kurejeshwa ili kuepusha nchi hiyo kuwa makaburi ya watu wasio na hatia.

Katika hatua nyingine wagombea watano wa urais nchini Guinea-Bissau wameendelea kulaani mapinduzi hayo ambayo yametekelezwa na Jeshi kwa madai serikali ilikuwa na mpango wa kupunguza ukubwa wa jeshi na hivyo wanajeshi wengine wangekosa kazi.

Wagombea hao wanaendelea kukosoa mapinduzi hayo wakati ambapo ujumbe maalumu toka ECOWAS ukiwa nchini humo na jana usiku walikuwa na mazungumzo na viongozi wa utawala wa kijeshi waliofanya mapinduzi.

ECOWAS imesema haitambui mapinduzi hayo na kwamba ujumbe huo umeenda nchini humo kwa lengo moja tu, la kuwashawishi wanajeshi waliotekeleza mapinduzi kuondoka madarakani na kurejesha utawala wa kiraia.

Jumuiya hiyo ya kiuchumi ya nchi za magharibi mwa Afrika pia imetishia kuiwekea vikwazo nchi hiyo endapo haitotekeleza kile ambacho kimekubaliwa na viongozi wa ECOWAS na ujumbe ambao wameutuma nchini Guinea-Bissau.

Nchi ya Guinea-Bissau imejikuta kwenye mgogoro toka kufariki kwa aliyekuwa rais wa nchi hiyo hiyo Malam Bacai Sanhna aliyefariki akiwa nchini Ufaransa akipatiwa matibabu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.