Pata taarifa kuu
GUINEA-BISSAU

Utawala wa kijeshi nchini Guinea-Bissau kutangaza baraza la Serikali ya mpito

Wanajeshi waliofanya mapinduzi nchini Guinea-Bissau hatimaye wamekubaliana na baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani nchini humo kuunda Serikali ya mpito kuandaa uchaguzi mkuu mwingine. 

Wanajeshi wa Guinea-Bissau wakiwa kwenye ofisi za Serikali punde baada ya mapinduzi
Wanajeshi wa Guinea-Bissau wakiwa kwenye ofisi za Serikali punde baada ya mapinduzi Reuters
Matangazo ya kibiashara

Viongozi hao wamekubaliana wakati huu ambapo mazungumzo kati ya utawala huo wa kijeshi na viongozi wa ECOWAS yakitarajiwa kuanza kujaribu kuushawishi utawala huo wakijeshi kurejesha utawala wa kiraia.

Uamuzi wa makubaliano hayo umetangazwa ikiwa ni saa chache zimepita toka utawala wa kijeshi nchini humo utangaze kufunga mipaka ya nchi hiyo pamoja na vituo vyote vya ndege.

Umoja wa nchi za magharibi ECOWAS umeendelea kulaani mapinduzi hayo ya kijeshi na kushinikiza kurejeshwa kwa Serikali ya kiraia ama nchi hiyo kukabiliwa na vikwazo vya kiuchumi.

Baraza jipya la Uongozi linatarajiwa kutangazwa siku chache zijazo baada ya vyama 22 kati ya 35 kukutana na kuwasilisha mapendekezo yao kwa utawala wa kijeshi.

Hata hivyo makubaliano hayo yanafanyika wakati ambapo baadhi ya vyama vya upinzani vimepinga mapinduzi hayo na kutaka shughuli nzima ya kupatikana kwa serikali mpya kuwa chini ya utawala wa Kiraia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.