Pata taarifa kuu
GUINEA-BISSAU

Wanajeshi wa Guinea-Bissau wafanya jaribio la Mapinduzi na kuteka Makao Makuu ya Chama Tawala

Vikosi vya Jeshi Nchini Guinea-Bissau vimefanya jaribio la mapinduzi kwa kushambulia Makazi ya Waziri Mkuu kisha kufuatiwa na tukio la kuwakamata baadhi ya wanasiasa pamoja na kuweka chini ya himaya yao makao makuu ya chama tawala nchini humo.

Waziri Mkuu wa Guinea-Bissau Carlos Gomes Junior ambaye anasakwa na wanajeshi waliotekeleza Mapinduzi
Waziri Mkuu wa Guinea-Bissau Carlos Gomes Junior ambaye anasakwa na wanajeshi waliotekeleza Mapinduzi
Matangazo ya kibiashara

Milio ya risasi ilisikika pamoja na milipuko ya maguruneti kwenye mitaani mbalimbali hasa katika Mji Mkuu Bissau kitu ambacho kilizua hofu kubwa kwa wananchi ambao walikuwa wanaendelea na shughuli zao za kawaida.

Jaribio hilo la Mapinduzi limetekelezwa wakati huu ambapo hakuna taarifa rasmi ambazo zinataja wapi ambapo yupo Waziri Mkuu anayeondoka madarakani na Mshindi wa duru la kwanza la kinyang'anyiro cha uchaguzi Carlos Gomes Junior.

Duru za Vikosi ambavyo vimetekeleza jaribio hilo la Mapinduzi zimesema wanaendelea kumsaka Waziri Mkuu Gomes Junior licha ya kutotambua eneo ambalo amehifadhiwa kwa sasa.

Licha ya Waziri Mkuu Gomes Junior kutotambulika alipo lakini pia Rais wa mpito wa nchi hiyo Raimundo Pereira hajulikani alipo licha ya askari wao watiifu kuweka bayana wapo sehemu salama na wataendelea kuwalinda.

Vikosi vingine vya jeshi vimeweka katika Kituo Cha Televisheni cha Taifa kudhibiti hatua yoyote ambayo inaweza kuchangia watu hao wakajitangazia utawala baada ya kutekeleza mapinduzi hayo.

Jumuiya ya Kiuchumi ya Mataifa ya Afrika Magharibi ECOWAS imelaani vikali mapinduzi hayo kwa kusema hayana baraka yoyote ya chombo hicho na wametaka serikali ya kiraia endelee kuiheshimiwa.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Cote D'Ivoire Daniel Kablan Duncan akizungumza kwa niaba ya ECOWAS amesema hawawezi kuunga mkono kile ambacho kimefanywa na wanajeshi waasi katika nchi ya Guinea-Bissau.

Wananchi wa Guinea-Bissau walikuwa wanaendelea kusubiri kufanyika kwa duru la pili la uchaguzi baada ya mchakato wa awali kushindwa kutoa mshindi ambaye alipata zaidi ya nusu ya kura zote licha ya upinzani kulalama uwepo wa wizi wa kura.

Uchaguzi huo uliitishwa baada ya kifo cha Rais Malam Bacai Sanha aliyefariki mwezi january mwaka huu baada ya Kiongozi huyo kuumwa kwa muda mrefu na kampeni za duru la pili zilikuwa zinatarajiwa kuanza leo na kufikia tamati tarehe ishirini na saba ya mwezi April.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.