Pata taarifa kuu
Senegal

Baraza la Mawaziri Senegal latangazwa, Youssou Ndour akwaa uwaziri

Mwanamuziki maarufu na mwanasiasa Youssou Ndour ni miongoni mwa mawaziri 25 katika serikali mpya ya Macky Sall nchini Senegal.

Pierre Rene-Worms
Matangazo ya kibiashara

Ndour ambaye sasa ni waziri wa utamaduni na utalii alimuunga mkono rais Sall wakati wa duru ya pili ya uchaguzi nchini humo, na ni miongoni mwa wanasiasa ambao pia walionesha nia ya kuwania urais nchini humo lakini hakufikia viwango vilivyohitajika na tume ya uchaguzi nchini humo.

Rais Sall amepunguza baraza la mawaziri hadi 25 kutoka idadi ya wali ya zaidi ya mawaziri 40 kama alivyoaahidi wakati wa kampeni zake.

Wachambuzi wa maswala ya kisiasa wanasema kuwa rais Sall kwa sasa anajaribu kuetekeleza yale yote aliyowaahidi wananchi wa Senegal wakati wa kampeni.

Serikali ya Macky Sall inakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo tatizo la ajira, huduma za jamii na mfumko wa bei.

Aidha Sall anakabiliwa na jukumu zito la kuhakikisha nchi hiyo inatawaliwa katika misingi ya kidemokrasia na kuhakikisha kuwa kunakuwa na utulivu na amani.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.