Pata taarifa kuu
Senegal

Senegal yapata waziri mkuu mpya, uchaguzi wa bunge wasogezwa mbele

Rais Mpya wa Senegal Macky Sall amemteua Abdoul Mbaye kuwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo huku mwenye akiendelea kusisitiza kipaumbele chake ni kurejesha amani na mshikamano baina ya wananchi wa taifa hilo.

REUTERS/Joe Penney
Matangazo ya kibiashara

Waziri Mkuu Mbaye atakuwa na jukumu la kuhakikisha serikali ya Rais Sall inatekeleza ahadi zote ambazo zilitolewa kwa wananchi wa Taifa hilo wakati wa kampeni za Urasi wa Duru la kwanza na lile la pili lililompa ushindi mbele ya Abdoulaye Wade.

Rais Sall amesema serikali yake haiwezi kukaa kimya kwa kile ambacho kinaendelea katika Mji wa Casamance kwa hiyo watapambana kurejesha utulivu katika eneo hilo.

Hatua hiyo ya Mack Sall inatoa matumaini mapya kwa wananchi Senegal baada ya utawala wa miaka 12 wa Bwana Abdoulaye Wade ambaye alilazimisha kubadilika kwa katiba ya nchi hiyo ili agombee katika kipindi kingine cha awamu ya tatu.

Mack Sall amesema kuwa uongozi maana yake ni kuwatumikia wale waliomchagua badala ya kufanya kazi kwa kuangalia maslahi binafsi na ana imani na Mbaye mwenye umri wa miaka 59 kuwa atatekeleza hayo.

Rais huyo mpya pia ametangaza kucheleshwa kwa uchaguzi wa bunge nchini humo na sasa utafanyika Julai 1 mwaka huu badala ya ijumaa Juni 17 akidai kuwa muda huo si mwafaka na amefanya hivyo kwa makubaliano na upande wa upinzani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.