Pata taarifa kuu
CONGO BRAZAVILLE

Watu 180 wathibitishwa kufa mpaka sasa nchini Congo Brazaville kufuatia tukio la kulipuka kwa ghala la silaha

Serikali nchini Congo Brazzaville imetangaza idadi mpya ya watu waliothibitishwa kufwa kwenye ajali ya milipuko ya ghala la silaha kuwa imefikia 180. 

Moja ya nyumba ambayo imebomoka kutokana na milipuko hiyo
Moja ya nyumba ambayo imebomoka kutokana na milipuko hiyo Reuters
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa afya wa nchi hiyo Georges Moyen amesema kuwa idadi hiyo huenda ikaongezeka kutokana na wengi wa majeruhi kuwa katika hali mbaya ya afya kutokana na majeraha ya kuungua.

Waziri huyo ameongeza kuwa idadi hiyo huenda ikaongezeka wakati huu ambapo juhudu za kuendelea kuwaska manusura na watu waliojeruhiwa zikiendelea kwa kushirikiana na mashirika ya kimataifa.

Zaidi ya watu elfu moja mia tatu na arobaini wamejeruhiwa katika tukio hilo la siku ya jumapili ambapo serikali imeahidi kuwalipa fidia wananchi ambao wamepoteza makazi na ndugu zao.

Waokojai toka mataifa ya Ufaransa, Morocco na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wamewasili nchini humo tayari kutoa msaada kwa serikali kuwasaidia wananchi ambao wameathirika na janga hilo.

Rais wa nchi hiyo Denis Sassou Nguesso ameendelea kutoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuisadia nchi hiyo wakati ambapo maelfu ya wananchi wanahitaji msaada wa haraka kunusuru maisha yao.

Kiongozi huyo hapo jana na leo alitembelea majeruhi walioko hospitali kuwajulia hali na kutoa msaada wa dawa kwenye hospitali ambazo zinawahudumia wahanga wa tukio hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.