Pata taarifa kuu
SOMALIA-UINGEREZA

Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza William Hegue atembelea nchi ya Somalia

Kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 21, serikali ya Uingereza imefungua rasmi ofisi za ubalozi wake mjini Mogadishu Somalia.

Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza William Hegue
Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza William Hegue UK defence
Matangazo ya kibiashara

Matt Baugh ndiye aliyetangazwa kuwa balozi mpya wa Uingereza nchini Somalia ambapo hii leo amewasilisha hati zake kwa rais wa nchi hiyo Sharif Sheikh Ahmed kwenye ikulu yake ya mjini Mogadishu.

Hii inakuwa ni mara ya kwanza kwa nchi ya Uingereza kufungua balozi yake toka iifunge miaka 21 iliyopita kutokana na kile ilichokieleza ni kuzorota kwa hali ya usalama kwenye nchi hiyo kufuatia mapigano na kundi la Al-Shabab.

Hata hivyo serikali ya Uingereza imesema kuwa kwasasa ofisi za balozi huyo mpya zitakuwa nchini Kenya mpaka pale hali ya usalama itakapotengamaa nchini humo.

Katika hatua nyingine waziri wa mambo ya nje wa Uingereza William Hegue amefanya zaira ya kwanza nchini Somalia katika kipindi cha miaka 20, na kutoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuongeza nguvu zaidi kukabiliana na wapiganaji wa kundi la Al-Shabab.

Ulinzi umeimarishwa mjini Mogadishu na maeneo mengine ambayo waziri huyo alifanya ziara ambapo wachambuzi wa mambo wanaona kuwa ziara hiyo inaanza kuonyesha juhudi mpya za Uingereza kutaka kuisaidia Somalia.

Waziri huyo amevipongeza vikosi vya Umoja wa Afrika AU kwa kufanikiwa kuwaondoa wapoganaji wa Al-Shabab kwenye mji mkuu Mogadishu na kutaka juhudi zaidi kufanywa ili kulitokomeza kabisa kundi hilo.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.