Pata taarifa kuu
Burundi

Burundi yaadhimisha miaka 18 tangu kuawa kwa kinara wa demokrasia Melchior Ndadaye

Burundi hii leo inaadhimisha kumbukumbu ya miaka 18 tangu kutokea kwa mauji ya hayati Melkior Ndadaye , kinara wa Demokrasia nchini humo. Melchior Ndadaye rais wa kwanza aliechaguliwa katika misingi ya kidemokrasia aliauawa usiku wa Octoba 21 mwaka 2003 na kundi la wanajeshi wa kitutsi wenye msimamo mkali ambao walishindwa kuvumilia kuona mtukutoka kabila la wahutu akiongoza nchi hiyo.

Amayagwa
Matangazo ya kibiashara

Melchior Ndadaye aliibuka mshindi kwenye uchaguzi wa mwezi Julai mwaka 2003 dhidi ya aliyekuwa rais wa nchi hiyo,pierre Buyoya chini ya chama chake cha SAHWANYA – FRODEBU. Ndadaye Hakupata muda wa kuongoza nchi hiyo kwani miezi mitatu tu baadae aliuawa, na hivyo kuibuka machafuko ya kikabila nchini humo, yaliosababisha watu zaidi ya laki nane kupoteza maisha huku wengine wakiitoroka nchi hiyo.

Mkatabwa wa amani na maridhiano uliosainiwa jijini Arusha, ndio uliowaleta pamoja kwa mara ya tena warundi. Mwaka 2005, Bunge la taifa hilo, lilipasisha sheria inayo mkubali Melchior Ndadaye kama kinara wa demokrasia nchini Burundi.

Kiongozi wa sasa wa chama hicho cha hayati Melchior Ndadaye, bwana Leonce Ngendakumana amesema anasikitika kuona misingi walioachiwa na kinara huyo ambayo ni udumishwaji wa demokrasia amani na utulivu nchini vimekuwa vikipewa kisogo.

Kama ilivyokuwa ada, viongozi mbalimbali wa serikali ya Burundi wamehudhuria misa ya kumuombea kiongozi huyo kwenye kanisa la Cathedrale Regina Mundi jijini Bujumbura.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.