Pata taarifa kuu
LIBYA

Rais wa Venezuela Hugo Chavez ashutumu mashambulizi ya NATO nchini Libya

Licha ya mashambulizi ya vikosi vya majeshi ya NATO nchini Libya kuendelea, rais wa Venezuela Hugo Chavez amemuandikia barua kiongozi wa Libya kanali Muomar Gadafi akimpongeza kwa ujasiri wake na kumuunga mkono kusalia madarakani.

Rais wa Venezuela Hugo Chavez
Rais wa Venezuela Hugo Chavez Reuters/Miraflores Palace/Handout
Matangazo ya kibiashara

Rais Chavez ambaye yupo nchini Cuba kwa matibabu ya saratani katika barua yake ameyashutumu vikali majeshi ya NATO yanayofanya operesehni nchini Libya akisema kuwa vita vyao havitafanikiwa dhidi ya serikali ya Libya.

Kiongozi huyo ndie ambaye amekuwa mtu wa karibu na Kanali Gaddafi huku akishutumu serikali ya waasi na kukosoa sera ya mambo ya nje ya Marekani akisema kuwa mataifa ya ulaya na Amerika yanapigana Libya kwa lengo la kutaka kujipatia mafuta.

Bado kumeendelea kuwa na uvumi toka katika ngome ya waasi kuwa mashambulizi ya NATO katika mji wa Ziltan yameua wanajeshi 30 wa serikali ya Gaddafi akiwemo mtoto wa kiongozi huyo Khamisi Gaddafi taarifa ambayo serikali imekanusha.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.