Pata taarifa kuu
MALAWI

Marekani yasitisha msaada wa fedha kwa nchi ya Malawi

Nchi ya Marekani imetangaza kusitisha mpango wake wa kutoa msaada wa fedha wa zaidi ya dola Milioni 350 ilizokuwa imepanga kuipatia nchi ya Malawi ili kuisaidia nchi hiyo kukabiliana na hali ngumu ya uchumi.

Rais wa Malawi Bingu wa Mutharika
Rais wa Malawi Bingu wa Mutharika Online
Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa iliyotolewa na ikulu ya Marekani, imesema kuwa nchi hiyo imeamua kufikia uamuzi huo kutokana na maandamano yanayoendelea nchini humo yaliyoshuhudia watu 19 wakipoteza maisha katika maandamano ya kupinga serikali ya rais Bingu wa Mutharik.

Aidha katika taarifa hiyo, nchi ya Marekani imeitaka Serikali ya Malawi kuzingatia na kulinda haki za binadamu ikiwemo kuruhusu demokrasia kwa wananchi wanaotaka kuandamana kwa amani kupinga hali mbaya ya uchumi.

Wakati Marekani ikitangaza kusitisha hatua ya kuipatia fedha nchi hiyo, rais Mutharika mwenyewe ameendelea kusisitiza kuzuia maandamano yoyote nchini humo na kuahidi kuwachukulia hatua viongozi walooko mafichoni wakihamasisha maandamano.

Hatua ya Marekani imekuja ikiwa zimepita siku chache tangu serikali ya Uingereza itangaze kusitisha msaada wa fedha katika bajeti ya Malawi na kusababisha kuzuka kwa maandamano kupinga serikali kusitisha pia mahusiano ya kibalozi na nchi hiyo.

Wanaharakati nchini humo wameipa serikali siku 21 kuhakikisha inatoa tamko kushuana na kutatua mgogoro wa uchumi unaoikumba nchi hiyo ikiwa ni pamoja na kuweka wazi mali za viongozi wa nchi hiyo ama sivyo wataitisha maandamano ya nchi nzima.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.