RFI Katuni za Meddy

Katuni hizi zinaashiria yale yanayoendelea kushuhudiwa ulimwenguni, ikiwa ni pamoja na kuzuiliwa kinyume cha sheria mwandishi wa habari wa RFI katika lugha ya Haousa nchini Cameroon Ahmed Abba.

Jumuiya ya Kimataifa imeshindwa kushtumu vikwazo vya Umoja aw Ulaya dhidi ya mgombea wa urais Emmanuel Shadary, Desemba 12, 2018.

Ufaransa: Emmanuel Macron anakabiliwa na waandamanaji wa vizibao vya njano ( 06/12/2018)

Kibonzo hiki kinaonesha wagombea wakuu wa upinzani Martin Fayulu na Felix Tshisekedi wakivutana kuelekea Uchaguzi wa urais mwezi Desemba, Novemba 28, 2018.

Saudi Arabia: Kibonzo hiki kinaelekea kauli ya rais wa Marekani Donald Trump kuwa Marekani haitachukulia hatua Saudi Arabia licha ya mauaji ya Jamal Khashoggi, Novemba 22, 2018.

Tanzania: Serikali katika juhudi za kunusuru zao la korosho kutoka kwa wazalishaji, Novemba 15, 2018.

Chama cha Republican kimeendelea kushikilia Baraza la Seneti, huku Bunge la wawakilishi likishikiliwa na chama cha Democratic, Novemba 2018.

Siku ya Kimataifa kupinga uhalifu dhidi ya wanahabari duniani 2/11/2018

Saudi Arabia yatambua kifo cha mwandishi wa habari Jamal Khashoggi katika ubalozi mdogo wa Istanbul, Oktoba 24 2018.

Uhusiano kati ya Marekani na Saudi Arabia waingia kasoro kufuatia kutowekwa kwa mwandishi wa habari Jamal Khashoggi, Oktoba 19, 2018!

Ndoa za utotoni ni chanagamoto kwa elimu ya wasichana, Oktoba 12, 2018.

Rwanda imeweka sheria mpya inayopiga marufuku katuni kwa maafisa wa serikali. Hukumu ya miaka miwili jela na faini ya zaidi ya dola 1000 imewekwa kwa yeyote atakaye kiuka sheria hiyo., Oktoba 4, 2018.

Ugonjwa wa Ebola utatishia kuingia Uganda ukitokea DRC pamoja na mashambulizi ya ADF katika ukanda huo, Septemba 27, 2018.

Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) ilimuhukumu kifungo cha mwaka mmoja kiongozi wa zamani wa kivita nchini DRC Jean-Pierre Bemba kwa kosa la kuhonga mashahidi, Septemba 19, 2018.

Raia wa Kenya wanalalamika kuhusu kupanda kwa kasi kwa bei ya mafuta tangu mwanzoni mwa mwezi huu, Septemba 13, 2018.

Mkutano wa 7 wa kiuchumi kati ya China na Afrika .. Beijing yaahadi uwekezaji wa dola bilioni 60 Afrika Septemba 4, 2018

Mwanamuziki na Mbunge wa upinzani nchini Uganda Bobi Wine, hatimaye ameachiliwa huru kwa dhamana baada ya kuwa rumande kwa muda wa wiki mbili, Agosti 29, 2018.

Zaidi ya wanamuziki mia moja wa kimataifa wanamuunga mkono mwanamuziki na mbunge Bobi wine anayekabiliwa na mashitaka ya uhaini, Agosti 23, 2018.

DRC: Emmanuel Ramazani Shadary aliyeteuliwa na Kabila kama mgombea urais katika uchaguzi wa urais wa Desemba 23, Agosti 18, 2018.

Sudan Kusini: Riek Machar na hasimu wake Salva Kiir wametia saini mkataba mpya wa amani, Agosti 6, 2018.

Wakati huu Jean-Pierre Bemba akirejea nyumbani, ataenda kuwa mgombea kwenye uchaguzi wa mwaka huu, 04/08/2018.

Mchakato wa kuchukua fomu za uchaguzi waanza DRC kuelekea uchaguzi wa Desemba 2018, Julai 26, 2018.

Ufaransa yaifunga Croatia katika fainali na kutwaa taji la Kombe la Dunia, Julai 15, 2018.

Eritrea na Ethiopia zafunua ukurasa mpya baada ya kukubaliana kusitisha vita vya miaka 20, Julai 11, 2018.

Kodi mpya kwa watumiaji wa mitandano ya kijamii nchini Uganda, 05 Julai, 2018.

USA-EU: Hatua za ulipizaji kisasi kwa kodi ya Marekani kuhusu uagizaji wa bidhaa za chuma na bati, Juni 26, 2018.

Siku ya Kimataifa ya Wakimbizi: Idadi ya wakimbizi inaendelea kuongezeka duniani kote, Juni 20, 2018.

Kim / Trump wajadiliana kuhusu mkataba wa nyuklia, Juni 12, 2018.

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu afanya ziara ya kikazi Ujerumani, Ufaransa na Uingereza kushawishi nchi hizi Ulaya kujitoa kwenye mkataba wa nyuklia wa Iran, Juni 6, 2018.

Kenya yapambana dhidi ya Rushwa wakati ambapo mamilioni ya dola yalizoibiwa kutoka Shirika la huduma kwa vijana (NYS), Mei 31, 2018.

Raia wa DRC wakiwa katika "vifungo viwili" katika mabega yao: Virusi vya Ebola na makundi yenye silaha yanayoendelea kuwa tishio. 24/05/2018

Burundi: Marekebisho ya Katiba yatashuhudia rais Pierre Nkurunziza akisalia madarakani hadi mwaka 2034. 17/05/2018

USA/Iran: Ingawa jumuiya ya kimataifa imefikia makubaliano na Iran ya kuacha uzalishaji wa vifaa vya nyuklia kwa matumizi ya kijeshi, Donald Trump ajitoa kwenye mkataba huu, Mei 9, 2018.

Siku ya kimataifa ya wafanyakazi, Mei 1, 2018.

Licha ya juhudi za bara la Afrika kutokomeza ugonjwa wa Malaria, bado ugonjwa huo unaua mamilioni ya raia

Kibonzo hiki kinaelezea uhuru wa matumizi wa mitandao ya kijamii ulivyo katika hatari ya kumomonyoka nchini Tanzania na Uganda.

Shambulio la kemikali nchini Syria laibua mvutano kati ya nchi za Magharibi na Urusi, Aprili 12, 2018.

Kim Jong UN alifanya ziara ya kushtukiza kwa Rais wa China Xi Jinping mwishoni mwa mwezi Machi wiki chache tu kabla ya mkutano na Marekani na Korea Kusini.

Kigali Mkutano wa AU: Nigeria yaonesha kutokuwa tayari kutia saini mkataba wa biashara huru kwa bara la Afrika. 21.03.2018

Kibonzo hiki kinaelezea rais wa Tanzania John Magufuli akiwaonya waaandamanaji kuwa serikali itakabiliana nao iwapo watajaribu kuandamana kuipinga serikali yake matamshi aliyotoa Machi 9 2018

Hayo ni miongoni mwa yale wanawake wanayokabiliana nayo katika maisha yao, Machi 8, 2018.

Marekebisho ya kikatiba Burundi: ukandamizaji dhidi ya wafuasi wa kura ya "hapana".

Wakimbizi wa DRC nchini Rwanda wanalalamika kuhusu mazingira yao ya maisha, Februari 22, 2018.

Afrika Kusini: Jacob Zuma, aliepotza imani ya chama chake, ajiuzulu, Februari 15, 2018.

Jacob Zuma aendelea kukabiliwa na shinikizo la kujiuzulu kutoka chama chake cha ANC, sasa yuko njia panda, akishikilia kamba nyembamba, Februari 7, 2018.

Raila Odinga ,mwanasiasa wa upinzania, aliyeshindwa katika uchaguzi wa urais alijiapisha mapema wiki hii kama raia wa wananchi wa Kenya, Januari 31, 2018.

Utawala wa Kabila nchini DRC unakabiliwa na maandamano kwa wito wa Kanisa Katoliki, Januari 25, 2018.

Rais wa Marekani Donald Trump hana imani na nchi za Kiafrika, Januari 18, 2018.

diapoflph_a_voir_egalement