Pata taarifa kuu
DRC-UCHUMI-UFISADI

Benki kuu ya DRC yaanza zoezi la kurejesha pesa zilizoporwa mwaka 2019

Benki kuu ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imethibitisha kwamba imeanza operesheni ya kurejesha fedha za umma zilizoporwa mwaka 2019. Hata hivyo benki hiyo inanyooshewa kidole cha lawama kwa hali hiyo.

Faranga za DR Congo (picha ya kumbukumbu).
Faranga za DR Congo (picha ya kumbukumbu). Capture d'écran du site du ministère congolais de RDC.
Matangazo ya kibiashara

Kwa karibu miezi mitatu, wafanyabiashara wanaouzia serikali bidhaa mbalimbali hawajalipwa, miradi mikubwa ya ujenzi imesitishwa ghafla na ofisi za serikali zinabaini kwamba zimechelewa kuwalipa wafanyakazi mishahara yao.

Operesheni hii inakuja kwa sababu ya wajibu wa mamlaka ya DRC wa kupunguza mfumko wa bei kati ya Oktoba na mwisho wa mwaka, mpango madhubuti ili kupata fedha kutoka Shirika la Fedha Duniani (IMF)wa dola milioni 360, kiwango ambacho taasisi ya Bretton Woods imekubali kutoa kati ya mwezi Desemba. Katika mteremko huu, Benki kuu ya DRC (BCC) imewekwa mashakani na wadau kadhaa, ikishutumiwa kwamba haikuwajibika kwa jukumu lake kama chombo kinachohusika na ukaguzi wa matumizi ya fedha za umma.

Kulingana na taarifa za RFI, Benki kuu ya DRC (BCC) iliipa serikali ya DRC dola milioni 360 (faranga bilioni 603) mwaka jana, kwa kukiuka kifungu cha 16 cha sheria hiyo kuhusu fedha za umma.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.