Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI-UFISADI-UCHUMI

Mahakama yafuta matokeo ya uchunguzi kwa watuhumiwa wa rushwa Afrika Kusini

Mahakama nchini Afrika Kusini imetupilia mbali matokeo ya uchunguzi uliowasafisha maafisa wa serikali kwa tuhuma za rushwa kuhusu manunuzi ya zana za kijeshi zilizogharimu mabilioni ya fedha, ambapo rais wa zamani Jacob Zuma alikuwa mtuhumiwa.

Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma wakati wa kesi yake kwenye mahakama ya Pietermaritzburg Novemba 30, 2018.
Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma wakati wa kesi yake kwenye mahakama ya Pietermaritzburg Novemba 30, 2018. ROGAN WARD / POOL / AFP
Matangazo ya kibiashara

Uchunguzi uliofanywa kwa miaka minne kuhusu kashfa ya ununuzi wa silaha, uliwekwa wazi mwaka 2016 na kuhitimisha kuwa hakukuwa na ushahidi wa kutosha kuthibitisha kulikuwa na makosa ya rushwa na udanganyifu.

Hata hivyo, mahakama mjini Pretoria inasema tume iliyochunguza kashfa hiyo ilifanya makosa makubwa ya kisheria kwa kukataa kupokea ushahidi wa nyaraka ambazo zilikuwa zinatuhuma mahsusi dhidi ya viongozi wa Serikali.

Duduzane Zuma, mtoto wa rais wa zamani wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, akiwasili kwenye mahakama ya Johannesburg inayoshughulikia kesi za ufisadi Julai 9, 2018.
Duduzane Zuma, mtoto wa rais wa zamani wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, akiwasili kwenye mahakama ya Johannesburg inayoshughulikia kesi za ufisadi Julai 9, 2018. REUTERS/Siphiwe Sibeko

Mahakama hiyo imesema wachunguzi pamoja na kuwahoji mashahidi muhimu katika kashfa hiyo, walishindwa kutumia muda wao kuhoji maswali ya msingi na yakina ambayo yangeweza kutoa ukweli.

Rais Zuma ambaye alilazimishwa kujiuzulu na chama chake cha ANC kutokana na kashfa za rushwa, pia anashtakiwa kwa makosa 16 yanayohusiana na manunuzi ya silaha hizo mwaka 1990 kabla hajawa rais.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.