Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI-UFISADI-UCHUMI

Afrika Kusini: Meya wa zamani wa Durban Zandile Gumede atimuliwa na chama chake

Hii ni kashfa nyingine ya ufisadi ambayo inakikabili chama tawala nchini Afrika Kusini, ANC. Manispaa ya jiji la Durban, mji wa tatu kwa ukubwa nchini Afrika kusini, inanyooshewa kidole cha lawama kwa kujihusisha na ubadhirifu wa mali ya umma.

Zandile Gumede, Meya wa mji wa Durban kwa miaka 3, alikuwa tayari amesimamishwa na kamati ya mkoa tangu mwezi Juni. (Hapa ilikuwa Septemba 2018).
Zandile Gumede, Meya wa mji wa Durban kwa miaka 3, alikuwa tayari amesimamishwa na kamati ya mkoa tangu mwezi Juni. (Hapa ilikuwa Septemba 2018). JOSH EDELSON / AFP
Matangazo ya kibiashara

Wakati huo huo Chama cha ANC chenye viti vingi bungeni kimeamua kumfukuza Meya wa mji wa Durban, Zandile Gumede.

Hivi sasa yuko chini ya uchunguzi wa utakatishaji fedha na rushwa katika kesi ya udanganyifu wakati wa kupata mkataba wa zabuni. Kashfa hiyo haimhusu Gumede pekee, lakini inawahusu pia madiwani zaidi ya sitini kutoka mkoa wa KwaZulu-Natal.

ANC imemaliza mgogoro unaodumu zaidi ya miezi miwili katika Manispaa ya jiji la Durban. Zandile Gumede, Meya wa mji huo kwa miaka mitatu, alikuwa tayari amesimamishwa na kamati ya mkoa tangu mwezi Juni. Na kwa sasa ametimuliwa kabisa na chama cha Cyril Ramaphosa.

Zandile Gumede na madiwani 62 wa manispaa ya jiji na mkoa wanatuhumiwa ubadhirifu wa mali ya umma.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.