rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Afrika Kusini Cyril Ramaphosa

Imechapishwa • Imehaririwa

Afrika Kusini: Cyril Ramaphosa ajibu mashitaka yamsimamizi wa mali za umma

media
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa katika mkutano na waandishi wa habari, Pretoria Julai 21, 2019. © Phill Magakoe / AFP

Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa amesema ataenda mahakamani kupinga ripoti ya ofisi ya msimamizi wa mali za umma ambayo ilimtaja kudanganya bunge kuhusu kupokea fedha za michango kusaidia kampeni yake mwaka 2017.


Ramaphosa amesema baada ya kuisoma kwa kina amebaini kuwa ripoti ile ina makosa na tuhuma za kupikwa na kutaka mara moja ifanyiwe mapitio na mahakama za nchi hiyo.

Kwenye ripoti hiyo Ramaphosa anadaiwa kupokea kiasi cha randi laki 5 kusaidia kampeni zake kinyume na maadili ya utumishi wa uma.

Tayari mkurugenzi wa ofisi ya usimamizi wa mali za umma, Busisiwe Mkhwebane ametoa taarifa akiunga mkono hatua iliyochukuliwa na rais Cyril Ramaphosa.