rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Marekani China Donald Trump

Imechapishwa • Imehaririwa

Trump atangaza kuongeza kodi ya Bilioni 200 kwa bidhaa kutoka China

media
Rais wa Marekani, Donald Trump, Januari 6, 2019 Washington. REUTERS/Joshua Roberts

Donald Trump ametangaza kuwa dola Bilioni 200 za bidhaa kutoka China ambazo hapo awali zilikuwa zikitozwa ushuru wa asilimia 10 zinapoingizwa nchini Marekani, kwa sasa zitatozwa ushuru wa 25% kuanzia Ijumaa.


Hatua hii inakuja kuweka shinikizo zaidi kwa China kwa lengo la kuhitimisha makubaliano ya biashara na Washington.

Hatua hii ya ghafla ya rais wa Marekani, ambaye hapo awali aliahirisha hatua ya kuongeza kodi, akibaini kwamba mazungumzo na China yanakwenda vizuri, inaonyesha kuongezeka kwa mvutano kati ya nchi hizi mbili zilizostawi kiuchumi duniani, wakati mazungumzo mapya yanatarajiwa kuanza wiki hii.

Kwa mujibu wa gazeti la Wall Street Journal, viongozi wa China wameshangazwa na hatua hiyo ya Trump na wanatarajia kufuta ziara ya Naibu Waziri Mkuu Liu He, anayeongoza mazungumza kwa upande wa China, ziara iliyokuwa imepangwa Jumatano wiki hii mjini Washington.

Wizara ya Biasha ya China haijatoa maelezo yoyote kuhusu hatua hiyo ya Marekani.