Pata taarifa kuu
AFRIKA-ULAYA-UCHUMI

Wataalamu: Ushirikiano wa kibiashara kati ya Afrika na Ulaya umepungua

Wataalamu wa masuala ya uchumi na biashara wanasema kuwa hali ya ufanyaji biashara baina ya nchi wanachama za Afrika imeongezeka huku ufanyaji biashara kati ya bara hilo na nchi za Ulaya ikipingua.

Katikati mwa jiji la Yaounde, mji mkuu wa Cameroon.
Katikati mwa jiji la Yaounde, mji mkuu wa Cameroon. Wikipédia
Matangazo ya kibiashara

Wakizungumza na idhaa ya Kiswahili ya RFI kando na mkutano wa kimkakati kuhusu fedha, uchumi na mipango, wataalamu wamesema bara la Afrika limepiga hatua kubwa katika ufanyaji biashara kati ya nchi wanachama huku ufanyaji biashara na nchi za Ulaya ukipingua.

Kwa mujibu wa ripoti iliyowasilishwa wakati wa mkutano huo, takwimu zinaonesha kuwa ufanyaji biashara kati ya nchi wanachama za Afrika umeongezeka kwa asilimia 20, huku biashara kati ya bara la Afrika na Ulaya ikipingua kwa asilimia 18.

Ushirikiano wa kikanda na uondolewaji wa vikwazo vya kibiashara ni kati ya mambo ambayo yameelezwa kuchangia kupanua wigo wa kibiashara baina ya nchi wanachama za Afrika.

Licha ya hatua kupigwa katika ufanyaji biashara na ushirikiano wa kikanda, changamoto ya masuala ya utawala bora na kukithiri kwa vitendo vya rushwa, ni sababu nyingine ambazo washiriki wa mkutano huu wanasema zinachangia pakubwa kuogeza hali ya umasikini kwa wananchi.

Issa Audu ni afisa kutoka benki kuu ya Nigeria, yeye anasema ni lazima bara la Afrika liwekeze katika kuimarisha miundombinu yake kwa kutilia mkazo elimu pamoja na kuhakikisha kuwa ukuaji wa uchumi wa mataifa ya Afrika unakuwa shirikishi.

Hata hivyo katika mkutano huo bado inaonekana baadhi ya nchi kutokuwa tayari kwenda na kasi iliyopo jambo, ambalo wataalamu wameonya kuwa litasababisha kuchelewa kwa utekelezwaji wa maazimio muhimu yanayolenga kubadili sura ya bara la Afrika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.