rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Eritrea Ethiopia Kenya

Imechapishwa • Imehaririwa

Nchi tatu za kanda ya Afrika Mashariki zakubaliana kuimarisha uchumi

media
Rais wa Eritrea Isaias Afwerki (kushoto) na Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed (kulia). REUTERS/GHIDEON MUSA ARON VISAFRIC

Ethiopia, Eritrea na Sudan Kusini zimekubaliana kuimarisha uchumi na siasa za mataifa hayo matatu kwa ajili ya maendeleo ya wananchi wake.


Makubaliano haya yamekuja, baada ya ziara ya Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed na rais wa Eritrea Isaias Afewerki jijini Juba, Jumatatu wiki hii na kufanya mazungumzo na rais Salva Kiir.

Ziara hii imekuja baada ya ziara nyingine kama hii kufanyika jijini Asmara kati ya rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na Waziri Mkuu wa Ethiopia, kuzungumzia ushirikiano wa kiuchumi.

Mbali na masuala ya uchumi, viongizi wa nchi hizo mbili, wamejadiliana pia kuhusu amani ya Sudan Kusini, hasa utekelezwaji wa mkataba wa kuundwa kwa serikali ya mpito kati rais Kiir na Riek Machar.