Pata taarifa kuu
MAREKANI-UCHUMI-SIASA

Trump adaiwa kusaidia familia yake kukwepa kodi

Rais wa Marekani Donald Trump anachunguzwa kwa madai ya kusaidia familia yake kukwepa kodi ya mamilioni ya dola katika miaka ya 1990. Hata hivyo Ikulu ya White House imetupilia mbali shutma hizo ikisema kuwa ni madai yasiokuwa na msingi.

Rais wa Marekani Donald Trump,achunguzwa kwa madai ya ukwepaji kodi.
Rais wa Marekani Donald Trump,achunguzwa kwa madai ya ukwepaji kodi. REUTERS/Kevin Lamarqu
Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa White House Sara Sanders amsema malipo yote yote yalikuwa yakipitishwa na kikaguliwa na mamlaka za kodi, kwa hivyo haikuwa rahisi Donald Trump kusaidifa familia yake kukwepa kodi.

Hata hivyo ripoti iliyochapishwa na gazeti la New York Times imemshutumu Rais Trump kwa kuhusika na mpango wa ulipaji kodi ili kujinufaisha yeye na familia yake.

Gazeti hilo la New York Times katika taarifa yake limesema pamoja na kwamba Rais Trump amekuwa akijinadi kuwa ubilionea wake unatokana na jitihada zake binafsi, lakini amekuwa akipokea mamilioni ya dola kutoka rasilimali za wazazi wake tangu akiwa na umri wa miaka mitatu.

Katika ripoti yake, gazeti la New york Times lisema fedha nyingi alizipata kutokana na kuwasaidia wazazi wake kukwepa kodi.

Gazeti hilo limesema Donald Trump na ndugu zake waliunda kampuni bandia na kujipatia mamilioni ya dola kama zawadi kutoka kwa wazazi wake.

Wakati huo huo mwanasheria wa Donald Trump, Charles Harder amekanusha madai hayo dhidi ya mtrja wake na kusema kuwa hakuna udanganyifu au ukwepaji wa kodi uliofanywa na mteja wake.

Hata hivyo amelishtumu gazeti la New Yprk Times akisema kuwa madai hayo ni uzushi, wala hayana msingi wowote.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.