Pata taarifa kuu
UINGEREZA-EU-UCHUMI

Wabunge 80 kupiga kura dhidi ya mpango wa May

Wabunge 80 wa chama cha Conservative nchini Uingereza wako tayari kupiga kura dhidi ya mpango wa Theresa May wa Uingereza kujitoa katika Umoja wa Ulaya, amesema Steve Baker, waziri wa zamani wa masuala ya Uingereza kujitoa katika Umoja wa Ulaya.

Chama cha Conservative chakumbwa na malumbano ya ndani Uingereza kufuatia mpango wa Theresa May wa kujitoa katika Umoja wa Ualya.
Chama cha Conservative chakumbwa na malumbano ya ndani Uingereza kufuatia mpango wa Theresa May wa kujitoa katika Umoja wa Ualya. REUTERS/Toby Melville
Matangazo ya kibiashara

Ikiwa Waziri Mkuu wa Uingereza ataendelea, anaweza kusababisha "hali ya taharuki " katika chama chake, ameongeza Steve Baker, ambaye alijiuzulu mnamo mwezi Julai mwaka huu.

Siku ya Jumapili, waziri wa zamani wa mambo ya nje, Boris Johnson alifananisha mpango wa Theresa May, uliyopitishwa mapema katika majira joto na "mkanda uliojaa vilipuzi" kando na Uingereza na "unasubiri tu kulipuliwa kwa muda wowote na Umoja wa Ulaya".

Steve Baker alitoa kauli hii mbele ya Chama cha Waandishi wa habari (Press Association) tarehe isiyojulikana. Alisema kuwa hapendelei kuwepo na mabadiliko ya uongozi, lakini Theresa May atakabiliwa na matatizo katika mkutano wa kila mwaka wa Chama cha Conservative uliopangwa kufanyika Septemba 30 hadi Oktoba 3.

Wafuasi wa Uingereza kujitoa katika Umoja wa ulaya wanaamini kwamba uchumi wa nchi hiyo utashamiri kwa muda wowote ule Uingereza itakua nje ya Umoja wa Ulaya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.