Pata taarifa kuu
DRC-EBOLA-AFYA

DRC: Watu tisa tayari wamefariki dunia kutokana na Ebola Beni

Idadi ya watu waliopoteza maisha kutokana na ugonjwa hatari wa Ebola katika Jimbo la Kivu Kaskazini, Mashariki mwa DRC imefikia tisa. Wizara ya afya nchini humo imesema watu wawili zaidi waliopoteza maisha walikuwa wakaazi wa Wilaya ya Beni.

Beni, mji mkuu wa mkoa wa Kivu Kaskazini ambako kesi mpya za Ebola zimegunduliwa.
Beni, mji mkuu wa mkoa wa Kivu Kaskazini ambako kesi mpya za Ebola zimegunduliwa. REUTERS/Samuel Mambo
Matangazo ya kibiashara

Hali hii imezua wasiwasi wakati huu serikali ikishirikiana na Shirika la afya duniani WHO ikianza kutoa chanjo kwa wakaazi wa Wilaya ya Beni.

Sampuli kutoka kwa wagonjwa 6 wanaopata matibabu zilichunguzwa na Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Biomedical, na kugundua kuwa 4 kati ya waathirika walikuwa na virusi vya Ebola.

Wataalamu wanajaribu kutathmini ni vipi ugonjwa huo umeanza kuenea tena katika ardhi ya DRC.

Ugonjwa huo hapo awali ulilipuka katika mkoa wa Equateur, kilomita zaidi ya 2500 kutoka Kivu.

Ebola ililipuka kwa mara ya kwanza nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo mnamo mwaka 1976.

Mataifa jirani, Uganda , Burundi, Tanzania na Rwanda yamesema yamechukua tahadhari kutokana na hali hii inayoendelea mashariki mwa nchi hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.