Pata taarifa kuu
TANZANIA-CHINA-UCHUMI-USHIRIKIANO

Rais wa Tanzania aiomba China kuwekeza zaidi Afrika

Rais wa Tanzania John Magufuli amesema licha ya mafanikio makubwa yaliyopatikana katika ushirikiano wa China na Afrika, bado kuna changamoto kubwa ya kukuza zaidi uhusiano katika masuala ya kiuchumi kwa kuhakikisha Afrika inauza bidhaa nyingi zaidi nchini China.

Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli.
Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli. REUTERS/Sadi Said
Matangazo ya kibiashara

Rais Magufuli ameitaka China kuongeza uwekezaji barani Afrika hususani katika kilimo, viwanda na madini, na pia kukuza ushirikiano katika ujenzi wa miundombinu ya usafiri na umeme.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo wakati akifungua mkutano maalum wa majadiliano kati ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na vyama vya siasa vya nchi mbalimbali za Afrika unaofanyika kwa siku mbili Jijini Dar es Salaam.

Ujumbe kutoka CPC umeongozwa na Waziri wa masuala ya uhusiano wa kimataifa wa CPC Song Tao na Afrika imewakilishwa na viongozi kutoka vyama takribani 40 vinavyojumuisha vyama vya ukombozi na ambavyo ni vyama rafiki wa CPC.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.