Pata taarifa kuu
EU-MAREKANI-BIASHARA-UCHUMI

Hatua za EU zaanza kutumika kufuatia ushuru wa Marekani

Umoja wa Ulaya umekua ukiitishia Marekani kuchukua hatua za kulipiza kisasi dhidi ya ushuru wa asilimia 25% kwenye bidhaa za chuma na 10% kwenye bati. Ijumaa hii, Juni 22, Umoja wa Ulaya umeamua kuchukua majibu dhidi ya hatua hiyo ya Marekani.

Mnamo Aprili 29, 2018, Emmanuel Macron, Theresa May na Angela Merkel walibanini kwamba  Umoja wa Ulaya (EU) hautokaa kimya kwa vikwazo vya kiuchumi vya Marekani kuhusu bidhaa za chuma na bati.
Mnamo Aprili 29, 2018, Emmanuel Macron, Theresa May na Angela Merkel walibanini kwamba Umoja wa Ulaya (EU) hautokaa kimya kwa vikwazo vya kiuchumi vya Marekani kuhusu bidhaa za chuma na bati. REUTERS/Francois Lenoir
Matangazo ya kibiashara

Ongezeko wa ushuru wa forodha kwenye mfululizo wa bidhaa kutoka Marekani umeanza kutumika.

Juisi ya machungwa, whisky, Harley Davidson ... orodha ya bidhaa zinazolengwa kutozwa ushuru wa 25% ni ndefu. Brussels inatoza ushuru kwenye bidhaa ya chuma na aluminium, sehemu ya tatu ya bidhaa nyingine za viwanda na theluthi moja ya bidhaa za kilimo kwa jumla ya euro bilioni 2.8 kwa uagizaji kutoka nje.

Ongezeko hili la tozo mpya ya EU kama hatua ya kujibu mapigo dhidi ya Marekani dhidi ya Marekani itaziathiri bidha kama tumbaku,piki piki maarufu za Harley Davidson, siagi ya karanga bidhaa ambazo kwa sasa zitakumbana na ongezeko la asilimia 25 sawa na kiasi cha euro bilion 2.8 ambapo utekelezwaji wake unaanza rasmi leo.

Umoja wa Ulaya unasema kuwa unataka kuwa makini sana kwa utawala wa Trump. Hata hivyo kwa mtazamo wa kwanza, akaunti haipo. Ushuru wa Marekani una thamani ya euro karibu bilioni 6 za mauzo ya Ulaya.

Rais wa jumuiya ya Ulaya Jean-Claude Juncker amesema tozo iliyoanzishwa na Marekani dhidi ya umoja huo inakwenda kinyume na hali halisi na historia ya uhusiano uliokuwepo kibiashara kati ya EU na Marekani.

Utekelezaji wa sera hiyo mpya ya biashara ya Marekani ilianza kutekelezwa june mosi na kuathiri mataifa kama vile Canada,Mexico na washirika wengine wa karibu kibiashara na Marekani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.