Pata taarifa kuu
TOGO-USALAMA-SIASA-UCHUMI

Mgogoro wa kisiasa waathiri uchumi Togo

Mgogoro wa kisiasa unaoendelea nchini Togo umesababisha mdororo wa kiuchumi, huku maduka yakiendelea kufungwa kutokana na hali mbaya ya kiuchumi. Raia wanaendelea kukabiliwa na hali mbaya ya kimaisha, huku mashirika mbalimbali yakiwataka wanasiasa, hasa serikali kutafutia ufumbuzi mgogoro huo.

Moja ya benki kuu mjini Lomé.
Moja ya benki kuu mjini Lomé. Danita Delimont/Gettyimages
Matangazo ya kibiashara

"Shughuli karibu zote zimezorota," amelaumu Seibu Issa, mfanyabiashara ambaye anamiliki moja ya maduka makubwa Deckon, eneo la kibiashara katika mji mkuu wa nchi hiyo ndogo Afrika Magharibi, Lome.

"Mauzo yangu yamepungua kwa zaidi ya nusu, kwa sababu wengi wa wateja wangu wanatoka nchi jirani, na hivi karibuni waliogopa kuja," anasema Issa.

Naye Paulo Azédjan, mfanyabiashara wa simu, anasema: "Ni vigumu sana, wateja wamekosekana kwa sasa na wafanyabiasha wakubwa wameanza kusafirisha biashara zao nchini Benin na Ghana, kwa sababu hali ya kiuchumi hapa nchini ni mbaya kabisa."

Tangu mwezi Septemba, makumi ya maelfu ya watu mara kwa mara wamekua wakiingia mitaani kwa kuitikia wito wa muungano wa vyama 14 vya upinzani, wakitaka Rais Faure Gnassingbe ajiuzulu. Faure Gnassingbe alichaguliwa kwa muhula mwengine mnamo mwaka 2010 na 2015 katika uchaguzi uliozua utata na kususiwa na upinzani, baada ya kumrithi baba yake aliyetawala nchi hiyo kwa kipindi cha miaka 38.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.