rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Uchumi Kenya

Imechapishwa • Imehaririwa

Tani 400 za sukari zamwagwa baharini Kenya

media
Serikali ya Kenya inasema itaendelea kuharibu bidhaa zitakazoingizwa nchini kinyume na sheria. Kauli hiyo imnakuja baadha ya kumwaga baharini tani 400 za sukari. Getty Images

Serikali ya Kenya mwishoni mwa juma lililopita ilimwaga baharini tani 400 za sukari iliyoingizwa nchini humo kimagendo kupitia bandari ya Mombasa kutoka nchini Dubai. Stakabadhi zilionyesha kuwa sukari hiyo ni kutoka nchini Brazil.


Kwa mujibu wa Waziri wa Viwanda nchini Kenya, Aden Mohammed, maafisa wa halmashauri ya ukusanyanji ushuru (KRA), waligundua makasha 16 yaliokuwa na sukari hiyo, ambayo nembo yailiyowekwa kwenye magunia ilionyesha kuwa imetengenezwa na kampuni ya sukari ya Kakira nchini Uganda.

Kwa upande wake Waziri wa Utalii, Najib Balala, amesema watashirikiana na taasisi mbalimbali kuhakikisha biashara isiyohalali inasitishwa nchini, ikiwa ni katika juhudi za kuboresha mapato ya taifa na kutoa ajira kwa Wakenya.

Naye Katibu wa biashara ya kimataifa, Chris Kiptoo, amesema aliyeingiza sukari hiyo nchini, aliaorodhesha mzigo wake kama mashini, hatua anayosema inanyima ushuru taifa na kurejesha nyuma wakulima wa miwa nchini kwa kuwa sukari hiyo huuzwa kwa bei ya reja reja nchini Kenya.

Shehena hiyo ya sukari ilikamatwa bandarini mwezi Februari mwaka uliyopita, huku mmiliki akiwasilisha kesi mahakani kupinga uharibifu huo, japo serikali inasema itaendelea kuharibu bidhaa zitakazoingizwa nchini kinyume na sheria.