rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Armenia

Imechapishwa • Imehaririwa

Uchaguzi mpya wa Waziri Mkuu kufanyika Mei 8 Armenia

media
Wafuasi wa upinzani nchini Armenia wakitikia wito wa Nikol Pachini wa kuendelea na maandamano na kuzuia barabara katika mji mkuu Erevan Mei 2, 2018 huko Erevan. REUTERS/Gleb Garanich

Uchaguzi wa waziri mkuu mpya nchini Armenia utafanyika Mei 8, Bunge la nchi hiyo limetangaza. Lakini upinzani umeapa kuendelea na maadamnano yao ya amani. Shughuli mbalimbali zimekwama katika mji mkuu wa nchi hiyo Erevan.


Jumanne wiki hii wabunge walishindwa kumchagua waziri mkuu mpya, ambaye alikua mgombea pekee kutoka upinzani, kiongozi wa upinzani na kiongozi wa maandamano ya tangu Aprili 13, Nikol Pashinian. Kufuatia hatua hiyo shughuli katika mji wa Erevan zimezorota

Ikiwa bunge litashindwa tena katika jaribio lake la kumchagua Waziri Mkuu, Bunge hilo litavunjwa na uchaguzi wa mapema wa wabunge utaitishwa.

Maandamano ya maelfu ya wapinzani yalisababishwa April 23 kujiuzulu kwa Serzh Sargsyan, ambaye alikuwa amechaguliwa tu muda si mrefu kama waziri mkuu, baada ya kuwa rais wa nchi hiyo kwa miaka kumi.

Siku ya Jumatano, mamia ya maelfu ya waandamanaji, kwa mujibu wa makadirio ya shirika la habari la AFP, wameingia mitaani katika mji wa Erevan kupinga hatua ya Bunge.