rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Zimbabwe Robert Mugabe

Imechapishwa • Imehaririwa

Mugabe aitishwa na bunge la Zimbabwe

media
Rais wa zamani wa Zimbabwe Robert Mugabe. Phill Magakoe / AFP

Rais wa zamani wa Zimbabwe, Robert Mugabe, ametakiwa kufika mbele ya bunge la nzhi hiyo mnamo Mei 9 kujieleza kuhusu "kutoweka kwa almasi zenye thamani ya dola bilioni 15," mbunge mmoja amesema.


"Tumeweka Mei 9 kama tarehe ambapo atatakiwa kutoa ushahidi," amesema Temba Mliswa, mwenyekiti wa Kamati ya Bunge inayohusika na maswala ya Madini na Nishati, akinukuliwa na gazeti la Herald.

"Kamati hiyo ilikutana leo [Alhamisi] na iliamua kumwalika rais wa zamani Robert Mugabe kwa kamati yetu ili kujieleza kuhusu kupoteza kwa almasi zenye thamani ya bilioni 15," ameongeza.

Mugabe, ambaye alitawala Zimbabwe tangu nchi hiyo kupata uhuru wake mwaka 1980, alilazimika kujiuzulu mnamo mwezi Novemba mwaka 2017chini ya shinikizo kutoka kwa jeshi, maandamano na chama chake, Zanu-PF.

Robert Mugabe ameiacha Zimbabwe katika hali ngumu kwa wananchi wake bila kusahau mgogoro wa kiuchumi unaoendelea.

Wabunge wanataka kumwuliza kuhusu maneno aliyotamka mwaka 2016, ambapo alielezea masikitiko yake kuwa nchi yake imepoteza dola bilioni 15 katika mapato ya almasi kwa sababu ya rushwa na kupotea kwa mitaji kutoka makampuni ya madini ya kigeni.

Kamati ya Bunge inayohusika na faili hii tayari imewataka mawaziri kadhaa wa zamani, wakuu wa polisi na maafisa wa ngazi ya juu serikalini kuja kutoa ushahidi.

Katika ripoti iliyotolewa mwaka jana, shirika lisilo lakiserikali la Global Witness limeshutumu viongozi wa Zimbabwe kupitisha mlango wa nyuma kwa miaka mingi faida ya madini ya almasi ili kufadhili ukandamizaji na wapinzani wao wa kisiasa.