rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Uingereza

Imechapishwa • Imehaririwa

Uingereza kuimarisha marufuku ya biashara ya pembe za ndovu

media
Uingereza inatarajia kuchukua hatua kali dhidi ya biashara ya pembe za ndovu. AFP

Uingereza inataka kuimarisha marufuku ya biashara ya pembe za ndovu, kuifanya moja ya sheria kali duniani, na hivyo kupambana dhidi ya ujangili wa tembo, Waziri wa Mazingira wa uingereza amesema leo Jumanne.


Wakati ambapo uuzaji wa vitu vinavyotengenezwa kwa pembe za ndovu kabla ya mwaka wa 1947 unaruhusiwa leo nchini Uingereza, serikali inatarajia kuwasilishwa bungeni muswada unaopiga marufuku kabisa uuzaji wa vitu vinavyotengenezwa kwa pembe za ndovu, bila kujali tarehe ambapo vilitengenezwa.

Uamuzi huu, ambao unatakiwa kupitishwa na Bunge, ulichukuliwa baada ya kushauriana na raia ambapo 88% ya washiriki 70,000 waliunga mkono marufuku hiyo.

Wahalifu watatozwa faini ya fedha zisizi kuwa ukomo na kukabiliwa na kifungo hadi miaka mitano.