rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

DRC

Imechapishwa • Imehaririwa

Chama cha UDPS chaendelea kukumbwa na malumbano

media
Jean-Marc Kabund (katikati) na FĂ©lix Tshisekedi (upande wake wa kushoto) katika mkutano na waandishi wa habari tarehe 2 Februari 2017, siku moja baada ya kifo cha Etienne Tshisekedi. Junior KANNAH / AFP

Chama kongwe cha upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo cha UDPS kinaendelea kukumbwa na malumbano ya ndani. Licha ya uchaguzi wa Felix Tshisekedi kukiongoza chama hicho, matokeo ya uchaguzi huo bado yanaendelea kupingwa.

 


Kundi linaloongozwa na Waziri Mkuu Bruno Tshibala, anayewakilishwa na Tharcisse Loseke, linaendelea kuwa na kutumaini kuwa matokeo ya mkutano mkuu wa chama cha UDPS ya tafutwa.

Wiki hii Mahakama ya mwanzo (TGI) ya Matete itaamua kuhusu ombi lililowasilishwa na kambi ya Tshibala ambayo ilipinga uamuzi uliosainiwa na katibu mkuu wachama cha UDPS wa kuitisha mkutano mkuu wa chama hicho .

Tharcisse Loseke, kiongozi wa kundi linaloongozwa na Waziri Mkuu Bruno Tshibala, ana matumaini kuwa mahakama itafuta matokeo ya uchaguzi ambapo Felix Tshisekedi alichaguliwa kuongoza chama cha UDPS.

Kwa upande wake na wanasheria wake, mkutano mkuu wa chama uliyoitishwa na Katibu Mkuu wa chama Jean-Marc Kabund uliopelekea uchaguzi kufanyika, ulikuwa kinyume cha sheria.

Paulin Mukala, rais wa kundi la wanasheria wa Tharcisse Loseke,anasema kwamba maamuzi yaliyochukuliwa katika mkutano mkuu wa chama yatafutwa na yatakuwa "hayana maana yyoyote".

Kwa upande wa UDPS inayoongozwa na Felix Tshisekedi, wanasema hawaoni kwanini mahakama inaweza kuipa sheria kambi ya Loseke-Tshibala.

Kambi nyingine ya tatu inayoongozwa na Valentin Mubake, imesem ahaitambui matokeo ya mkutano mkuu. Siku ya Alhamisi iliyopita, Tume ya kitaifa inayofuatilia makubaliano (CNSA) iliamua na kutaja kuwa uamuzi wa UDPS inayoongozwa na katibu mkuu Jean-Marc Kabund ulikua sahihi.

CNSA iliitaka kambi ya Tshibala-Loseke kuunda chama kipya na kuchagua chenye jina tofauti na UDPS. Agizo hilo lilitolewa pia kwa kwa Valentin Mubake na Corneille Mulumba.