Pata taarifa kuu
CHINA-MAREKANI-BIASHARA

Bidhaa 128 za Marekani kutozwa kodi China

China imetangaza leo Jumatatu Aprili 2 hatua za kulipiza kisasi dhidi ya uagizaji wa Marekani kwa kutoza kodi bidhaa zake 128, zenye thamani ya dola bilioni 3, kwa kukabiliana na kodi ya Marekani kuhusu madini ya chuma na aluminium, kwa mujibu wa shirika la habari la Chine nouvelle.

Rais Trump na mwenzake wa China Xi Jinping, Novemba 9, 2017 Beijing.
Rais Trump na mwenzake wa China Xi Jinping, Novemba 9, 2017 Beijing. Reuters/路透社
Matangazo ya kibiashara

Mwezi uliopita, Beijing ilionya kuwa inatafakari kuanzisha utaratibu wa kutoza kodi baadhi ya bidhaa kutoka Marekani, na hivyo kuzua wasi wasi ya kutokea kwa vita vya kibiashara kati ya nchi hizi mbili zilizostawi kiuchumi duniani. Kodi hizi mpya za China, zilizowekwa na tume ya ushuru katika, zinalenga bidhaa mbalimbali kutoka kwa matunda hadi nyama nguruwe.

"Vitisho vya kiuchumi"

Mnamo Machi 22, Rais wa Marekani Donald Trump alitangaza kuwa Marekani itaweka kodi mpya kwa bidhaa kutoka China zenye thamani ya dola bilioni 60, taarifa ambayo ilizua sintofahamu kwenye masoko mbalimbali. Siku iliyofuata, China ilijibu kwa kufichua orodha ya bidhaa 128 ambazo ilisema zitatakiwa kulipiwa ushuru kutoka 15% hadi 25% ikiwa nchi hizi mbili zitashindwa kuafikiana.

Washington inashutumu China kwa muda mrefu kunufaika na mfumo wa pamoja wa ubia unaowekwa kwa makampuni ya kigeni nchini China ili kupoteza uvumbuzi wa teknolojia ya Marekani. China imeiomba Marekani kuachana na kile ilichokiita "vitisho vya kiuchumi", na kutishia kulipiza kisasi.

Lakini mpaka sasa, China imejizuia kuchukukua hatua dhidi ya bidhaa mujimu vya kilimo, kama vile soya, au dhidi ya makampuni makubwa ya viwanda kama vile Boeing, sekta ambazo pia zilitakiwa kulengwa, gazeti la serikali la kila siku la Global Times limebaini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.