Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI-SIASA

Bunge la Afrika Kusini lamchagua Cyril Ramaphosa kuwa rais mpya

Bunge nchini Afrika Kusini limemchagua bila kupingwa Cyril Ramaphosa kuwa rais mpya wa taifa hilo akichukua nafasi ya Jacob Zuma aliyetangaza kujiuzulu nafasi yake usiku wa kuamkia leo.

Cyril Ramaphosa, rais mteule wa Afrika Kusini, wakati wa hotuba yake mbele ya Bunge, Februari 15, 2018.
Cyril Ramaphosa, rais mteule wa Afrika Kusini, wakati wa hotuba yake mbele ya Bunge, Februari 15, 2018. REUTERS/Mike Hutchings
Matangazo ya kibiashara

Makamu wa rais akiwa pia kiongozi wa chama tawala cha ANC nchini Afrika Kusini Cyril Ramaphosa ameapishwa kuwa rais wa Afrika Kusini baada ya Jacob Zuma kujiuzulu hapo jana Jumatano.

Tangu achukue hatamu ya uongozi wa chama, Bw Ramaphosa alikua akimsihi mtangulizi wake kujiuzulu, biila mafanikio.

Uamuzi wa kujiuzulu wa zuma ulikua baada ya chama chake kutishia kuwasilisha bungeni muswada wa kutokua na imani dhidi yake. Muswada ambao ungewasilishwa leo, kama Jacob hangelijiuzulu.

Hata hivyo katika hotuba yake iliyorushwa moja kwa moja kwenye televisheni Bw zuma alisema kuwa chama cha ANC hakijamtendea haki kwa kumtaka ajiuzulu bila sababu zozote.

Jacob Zuma anakabiliwa na kashfa za rushwa. Kwa mujibu wa chanzo kutoka chama cha AHC, hiyo ni moja ya sababu zilizomponza Bw Zuma.

Bwana Zuma ,mwanachama wa jeshi la ANC wakati wa ubaguzi wa rangi, alipitia nyadhfa kadhaa za chama hicho hadi kuwa rais.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.