Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI-SIASA-UCHUMI

Jacob Zuma: Chama cha ANC hakijanitendea haki

Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma anaendelea kusema kuwa hajafanya chochote kibaya. Amerejelea mara kadhaa kauli hiyo kwenye televisheni ya taifa ya SABC, alipokua akitoa moja kwa moja msimamo wake kufuatia uamuzi wa chama chake kumtaka ajiuzulu mara moja.

Jacob Zuma, rais wa Afrika Kusini.
Jacob Zuma, rais wa Afrika Kusini. REUTERS/Siphiwe Sibeko
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa Rais Zuma ambaye alionekana kwenye televisheni akisegemea ukuta, amesema, wito wa chama chake cha ANC kutaka ajiuzulu sio "sahihi".

"Wakati wa majadiliano, ilikua kama kawaida tu watu kusema 'Zuma lazima aondoke'. Kauli hii sio mpya. Hii imesemwa mara nyingi kwa mwaka mzima. Lakini watu hawa hawajatoa sababu zao. Ndiyo sababu ninastaajabishwa na chama changu kunambia: 'Sasa unapaswa kuondoka madarakani', bila hata hivyo kkufuata taratibu za chama cha ANC, "RAis Zuma amesema kwenye runinga ya taifa ya SABC. "Sio sahihi kuona mada hii inaendelea kuzua hali ya sintofahamu," ameongeza.

Baada ya wito rasmi wa kumtaka ajiuzulu jana Jumanne, chama cha ANC kimeamua kuongeza shinikizo. Kutokana na ukimya wa Jacob Zuma, chama hicho kimeamua kutumia njia muhimu. "Ni wazi sasa kwa viongozi wa ANC kutoweza kusubiri zaidi ya leo. Hatuwezi kuwafanya raia wa Afrika Kusini kuendelea kusubiri. Ikiwa Rais Zuma atna nia ya kujibu, basi atajibu. Lakini hatuwezi kusubiri tena, "amesema Muweka hazina wa ANC Paul Mashatile. Chama cha ANC tayari kimewasilisha bungeni leo asubuhi barua ya kutokua na imani na rais Zuma. Suala hilo litajadiliwa kesho Alhamisi.

Zuma tayari ameponea chupuchupu kwa kura ya kutokua na imani naye bungeni kutokana na chama chake chenye wajumbe 249 kati ya 400 katika bunge la Afrika Kusini.

Jacob Zuma anaonekana anjaribu kupoteza muda. Baada ya wiki kadhaa za majadiliano, raia wa Afrika kusini wameanza kukata tamaa kuhusu kujiuzulu kwa Rais Zuma.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.