rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Uingereza

Imechapishwa • Imehaririwa

Uwanja wa ndege wa London City wafunguliwa

media
Safari za ndege zaruhusiwa tena katika uwanja wa ndege wa London City, Uingereza. AFP

Mamlaka ya uwanja wa ndege wa London City imeamua kufungua uwanja huo ulio karibu na eneo la katikati la mji mkuu wa Uingereza.


Hatua hii inakuja siku moja baada ya bomu la vita vya pili vya dunia kupatikana kwenye mto ulio karibu wa Thames.

 

Kikosi cha kutegua mabomu kilifanikiwa kuondoa bomu hilo la Ujerumani, bomu la vita vya pili vya dunia, lenya uzito wa nusu tani.

"Uwanja wa ndege utafunguliwa kesho Jumanne, " ametangaza Mkurugenzi wa mamlaka ya uwanja wa ndege, Robert Sinclair katika taarifa yake.

Uwanja huo ulifungwa siku nzima na safari zote za ndege kufutwa, na kuwaathiri hadi abiria 16,000.

Baadhi ya ndege zililazimika kutua kwenye uwanja wa Stansted na Southend.