rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Uhispania

Imechapishwa • Imehaririwa

Madrid kuzuia uchaguzi wa Puigdemont Catalonia

media
Aliyekua rais wa Catalonia Carles PuigdemontDisemba 17, 2017. Fuente: Reuters.

Serikali ya Uhispania imeanzisha mchakato ili kuzuia uchaguzi wa Carles Puigdemont kama rais wa serikali ya Catalonia, makamu wa rais wa serikali ya Madrid, Soraya Saenz de Santamaria, amesema leo Alhamisi.


Serikali imeomba Halmashauri kuu ya Serikali kutoa maoni yake juu ya uwezekano wa kukata rufaa kwenye Mahakama ya Katiba kuhusu uamuzi wa Bunge la Catalonia kumteua Carles Puigdemont kama mgombea pekee wa urais wa Catalonia, Soraya Saenza de Santamaria amesema katika mkutano na waandishi wa habari.

Ikiwa maoni ya Halmashauri kuu ya Serikali yatakua yataruhusu kufanya hivyo, rufaa hii itawasilishwa mara moja, amesisitiza Soraya Saenz de Santamaria.

Bw Puigdemont aliyekimbilia uhamishoni nchini Ubelgiji tangu mwishoni mwa mwezi Oktoba, anaweza kukamatwa na kuzuiliwa kwa kosa la "uasi", "uchochezi" na "ufisadi" ikiwa anarejea Uhspania.

Alipendekezwa siku ya Jumatatu iliyopita kuwa mgombea wa urais wa Catalonia. Kura imepangwa kufanyika Januari 31.

Wafuasi wake wamependekeza kwamba aongoze Catalonia akiwa Brussels kupitia kiunganisho cha video, hoja ambayo imepuuziwa mbali na rais wa serikali ya Uhispania Mariano Rajoy.

Waziri wa mambo ya ndani wa Uhispania, Juan Ignacio Zoido, alisema siku ya Jumanne kuwa vikosi vya usalama vimezidisha ulinzi ili kuzuia Carles Puigdemont kurudi Catalonia, "kwa helikopta, kwa treni, kwa gari au kwa meli"