rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Uchumi Ufaransa Uswisi Emmanuel Macron

Imechapishwa • Imehaririwa

Macron: Ufaransa inataka mkataba mpya wa kimataifa

media
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, Davos Januari 24, 2018. REUTERS/Denis Balibouse

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ametaka mataifa ya dunia yenye uchumi mkubwa kubadilisha sare zake za kiuchumi na kiviwanda ili kukaribisha wawekezaji zaidi kutoka nje.


Akiwahotubia viongozi wa dunia katika jukwaa la kiuchumi jijini Davos nchini Uswisi, rais Macron amesema mabadiliko ya sera ya kichumi, yatasaidia kuunda nafasi za ajira.

Aidha, ametoa wito wa mshikamano zaidi katika Umoja wa Ulaya.

"France is Back", "Ufaransa inarudi", alisema rais wa Ufarasa Emmanuel Macon, huku akishangiliwa na viongozi mbalimbali wanaohudhuria mkutano kuhusu masuala ya kiuchumi unaoendelea Davos nchini Uswisi, ambako pia aliomba "mkataba mpya wa kimataifa".

"Ilikua marufuku kushindwa nchini Ufaransa na haramu kufanikiwa," alisema rais wa Ufaransa katika hotuba yake aliyota katika mkutano kuhusu masuala ya kiuchumi, huku akikihimiza "kuchukua tahadhari". Rais Macron alizungumzia kwa kina mageuzi yake kwa lugha ya Kiingereza.

Baadae rais wa Ufaransa aliendelea kutoa hotuba yake kwa Lugha ya Kifaransa akiomba "mkataba mpya wa kimataifa" kwa utandawazi "ambao unavuta dunia kuelekea kuangamia." Vinginevyo, alionya, "uchochezi au misimamo mikali itaweza kushinda miaka 10 au 15 katika nchi zote. "

Emmanuel Macron ametoa wito kwa makampuni ya kimataifa, ambayo mengi yalituma wajumbe wao kuhudhuria mkutano huo "kuachana kupandisha kodi kwa gharama yoyote."

Serikali inapaswa kuwa na "mikakati ya kodi inayotolewa katika kiwango cha kimataifa", hasa kwa kutoza makampuni makubwa "ambao hayalipi kodi," alisema Rais Macon.