rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Venezuela Nicolas Maduro

Imechapishwa • Imehaririwa

Maduro kuwania katika uchaguzi wa urais nchini Venezuela

media
Rais Nicolas Maduro anasema yuko tayari kuwania katika uchaguzi mwaka huu. Miraflores Palace/Handout via REUTERS

Bunge nchini Venezuela limetaka kufanyika kwa Uchaguzi mpya kabla ya mwezi Aprili mwaka huu. Uamuzi huo umeungwa mkono na rais Nicolas Maduro ambaye amewaambia wafausi wake kuwa yuko tayari kwa uchaguzi huo.


Aidha, amesifu uamuzi huo wa bunge na kusema, utasaidia kuwazuia maadui wa nchi hiyo anaosema wanataka kuharibu uchumu wa Venezuela.

Mnamo mwezi Oktoba mwaka jana Upinzani nchini Venezuela uligomea matokeo ya uchaguzi

Upinzani ulikataa kuyatambua matokeo ya uchaguzi wa majimbo uliompa ushindi mkubwa Rais Nicolas Maduro na chama chake kinachoelemea siasa za mrengo wa kushoto, wakiitisha maandamano kudai kuhisabiwa upya kura.

Hata kabla ya Tume ya Uchaguzi kutangaza matokeo hayo, muungano wa upinzani ujiitao Mshikamano wa Kidemokrasia ulidai kwamba ulikuwa na taarifa za tume hiyo kuyachezea matokeo halisi ya kura.

Lakini awali Tume ya Uchaguzi iliuthibitisha muungano wa upinzani kushinda viti vingi vya ubunge nchini humo.

Mnamo mwezi Aprili mwaka jana Rais wa Venezuela Nicolas Maduro aliitisha kurejelewa kwa mazungumzo kati ya serikali na upinzani nchini humo.

Upinzani unailaumu serikali kwa mgogoro wa kiuchumi ambao umeathiri pakubwa nchi hiyo na kusababisha uhaba wa vyakula, bidhaa muhimu na dawa.