Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI-ZUMA-SIASA-UCHUMI

ANC: Tunajadili utaratibu wa kumng'atua madarakani Zuma

Chama tawala nchini Afrika Kusini ANC, kimethibitisha kuwa kinajadili kuondoka madarakani kwa rais Jacob Zuma. Hata hivyo, haijakubaliwa tarehe rasmi ya kuachia madaraka jkwa rais Zuma, kuelekea Uchaguzi Mkuu mwaka ujao.

Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma.
Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma. © REUTERS/Nic Bothma/Pool/Files
Matangazo ya kibiashara

Duru kutoka ndani ya chama hicho, zimesema kuwa rais Zuma ambaye anatuhumiwa kuhusika na matukio mbalimbali ya ufisadi ameshauriwa kujiuzulu mwenyewe la sivyo ataondolewa kwa nguvu na chama hicho.

Shinikizo zimekua zikiongezeka kwa rais Jacob Zuma kutakiwa kujiuzulu nafasi yake kabla ya uchaguzi mkuu wa hapo mwakani.

Hivi karibuni Bunge nchini Afrika Kusini lilitangaza kuwa linatazamia kujadili hatua za kuchukua kumuondoa rais Zuma Madarakani.

Uamuzi huu wa bunge ulikuja ikiwa ni siku chache tu zimepita toka mahakama ya katiba nchini humo kuamua kuwa bunge lilishindwa kumuwajibisha rais Zuma kwa matumizi mabaya ya fedha za umma kufanya ukarabati kwenye makazi yake binafsi.

Miezi miwili iliyopita mahakama ilimkuta na hatia ya kukiuka hati ya kiapo kwa kukataa kurejesha kiasi cha fedha alichotakiwa kurudisha na kuliagiza bunge kuandaa mchakato utakaotumika kumuondoa madarakani.

Rais Zuma anaendelea kukabiliwa na kashfa ya ufisadi, huku chama cha Nelson Mandela kikiendelea kupoteza wafuasi katika majimbo mbalimbali nchini humo.

Julius Malema mkosoaji na mpinzani mkubwa wa Jacob Zuma amekua akihamasisha wabunge wenzake kuchukua uamuzi wa kumng'atua madarakani, bila mafanikio.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.