Pata taarifa kuu
LIBERIA-SIASA

George Weah atawazwa kama rais wa Liberia

Nyota wa zamani wa soka George Weah ameapishwa leo Jumatatu kama rais wa Liberia mbele ya maelfu ya wafuasi wake, ikiwa ni zoezi la kwanza wa kukabidhiana madaraka kati ya marais hawa wawili waliochaguliwa nchini humo tangu 1944.

Rais mpya wa Liberia, George Weah, na Rais anayemaliza muda wake Ellen Johnson Sirleaf wakati wa sherehe za kukabidhiana madaraka Januari 22, 2018.
Rais mpya wa Liberia, George Weah, na Rais anayemaliza muda wake Ellen Johnson Sirleaf wakati wa sherehe za kukabidhiana madaraka Januari 22, 2018. REUTERS/Thierry Gouegnon
Matangazo ya kibiashara

George Weah ameapishwa leo mchana mbele ya Mkuu wa Mahakama Kuu Francis Korpor, katika uwanja mkubwa wa mji mkuu wa Monrovia, uliofurika watu, waandishi wa habari wa shirik ala habari la AFP wamearifu.

Akihutubu baada ya kula kiapo, Bw Weah amesema:"Nitafanya zaidi ya mchango ninaotarajiwa kutoa ili kutimiza matarajio yenu - lakini naomba nanyi mtimize matarajio yangu, siwezi kutimiza haya peke yangu."

George Weah anamrithi Ellen Johnson Sirleaf, mwanamke wa kwanza aliyechaguliwa rais barani Afrika mwaka 2005.

Maelfu ya raia wa Liberia wakiwemo marais kadhaa hasa kutoka Afrika Magharibi wanmehudhuria sherehe hizo.

Mbali na viongozi wa mataifa ya Afrika, wachezaji wa mchezo wa soka kama Didier Drogba na Samwel Eto'o miongoni mwa wengine wamehudhuria sherehe hiyo.

Mwishoni mwa wiki iliyopita, mchezaji huyo zamani wa mchezo wa soka, alisema kazi yake kubwa itakuwa ni kuhimiza amani nchini humo.

Kuapishwa kwa Weah kunamaliza, uongozi wa rais Ellen Johnson Sirleaf ambaye amekuwa akiongoza nchi hiyo tangu mwaka 2005.

Bi.Sirleaf anaondoka akiwa na rekodi nzuri ya kuhimiza amani nchini humo baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyosababisha vifo vya watu wengi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.