Pata taarifa kuu
SUDAN-MAANDAMANO-UCHUMI

Maelfu ya raia kumiminika mitaani kwa mara nyingine nchini Sudan

Waandamanaji nchini Sudan wameanza tena kujitokeza katika miji mbalimbali kulalamikia kupanda kwa bei ya vyakula nchini humo hasa mkate.

Raia wa Sudan waendelea kuandamana kupinga kupanda kwa bei ya vyakula, hasa mkate.
Raia wa Sudan waendelea kuandamana kupinga kupanda kwa bei ya vyakula, hasa mkate. REUTERS/Stringer
Matangazo ya kibiashara

Jana Jumatano polisi wa kupambana na ghasia walikabiliana na mamia ya waandamanaji katika mji wa Omdurman.

Maandamano haya yamepangwa na chama kikuu cha upinzani cha UMMA, na yanatarajiwa kuendelea kwa mujibu wa wanasiasa wa upinzani.

Tangu kuzuka kwa maandamano hayo, watu kadhaa wamekamatwa na wengine wamejeruhiwa bila kusahau watu waliopoteza maisha yao.

Polisi nchini Sudan imeendelea kulaumiwa kwa kutumia nguvu kupita kiasi kwa kusambaratisha maandamano hayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.