Pata taarifa kuu
DRC-UBELGIJI-USHIRIKIANO-UCHUMI

Ubelgiji kusitisha misaada yake kwa DRC

Ubelgiji imetangaza kuwa imerejelea upya ushirikiano wake na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na hata kuzungumzia marekebisho ya msingi. Ubelgiji imetishia hata kusitisha misaada yake kwa serikali.

Kwa upande wa mashirika yasiyo ya kiserikali sawa na Bunge la Ulaya, wamekua wakiomba DRC ichukuliwe vikwazo vya kiuchumi
Kwa upande wa mashirika yasiyo ya kiserikali sawa na Bunge la Ulaya, wamekua wakiomba DRC ichukuliwe vikwazo vya kiuchumi Eddy LEMAISTRE / Contributeur / Getty Images
Matangazo ya kibiashara

Dola milioni 25 ambazo zingelipaswa kutolewa katika sekta zinazosimamiwa na serikali ya DRC zitatolewa katika mipango ya misaada ya kibinadamu au kusaidia mashirika ya kiraia nchini DRC.

Kwa upande wa mashirika yasiyo ya kiserikali sawa na Bunge la Ulaya, wamekua wakiomba DRC ichukuliwe vikwazo vya kiuchumi. Bunge la Ulaya linatarajiwa kujadili azimio la dharura kuhusu DRC siku ya Alhamisi Januari 18, huku likiomba Umoja wa Ulaya kuwa makini zaidi na hali ya kibinadamu inayojiri nchini DRC.Lakini suala hili si rahisi kulitatua.

Masuali abayo yamekua yakiulizwa ni je Umoja wa Ulaya unaweza kufuata mfano wa Ubelgiji? Hapana, amejibu afisa wa Umoja wa Ulaya, hakuna muingiliano kuhusu suala hilo, msaada wa maendeleo unasimamiwa katika mfumo wa Mfuko wa Ulaya wa Maendeleo. Msaada wa kibinadamu unakabidhiwa shirika la lisilo la kiserikali la Echo, na wafadhili ni Umoja wa Ulaya.

Mkurugenzi wa Echo anatazamiwa kuzuru katika siku zijazo DR Congo wakati ambapo mpango wa utekelezaji wa misaada ya kibinadamu uko katika kiwango cha chini cha fedha tangu miaka 10 iliyopita. Kwa upande wa hirika lisilo la kiserikali la EDF, mipango inayohusiana na utawala, haki na polisi, tayari umesimamishwa, kwa mujibu wa chanzo cha kidiplomasia cha Umoja wa Ulaya. Umoja wa Ulaya, kwa upande mwingine, inaendelea na mipango yake kuhusu viumbe hai na miundombinu.

Kwa mujibu wa vyanzo kadhaa, Ubelgiji imeanzisha mchakato ili kupata uhakikisho wa DRC kuchukuliwa vikwazo vigumu vya kiuchumi. Ubelgiji inataka kuishawishi Marekani, Ufaransa na Uhispania. "Tumejaribu hatua hii ngumu kwa Burundi, matokeo yake yamegonga mwamba, haina maana kuchukua hatua kama hizo," kimesema chanzo cha kidiplomasia cha Ufaransa ambacho imekumbukumbusha umuhimu wa kuendelea na mchakato wa mazungumzo na serikali ya Kinshasa. "Wanasema hivo kwa sababu Ufaransa na Uhispania wanatafuta mikataba nchini DRC," mmoja miongoni mwa wanaharakati nchini DRC ameshtumu. Huu ni uongo, chanzo cha kidiplomasia cha Ufaransa kimesema. "Tunapaswa kuweka kipaumbele suluhisho la pamoja na Umoja wa Afrika na nchi za Ukanda," kimeongeza chanzo hiki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.