Pata taarifa kuu
TUNISIA-MAANDAMANO-UCHUMI

Wananchi wajitokea mitaani kwa mara nyingine Tunisia

Serikali ya Tunisia inasema, idadi ya watu waliokamatwa kutokana na maandamano yanayoendelea nchini humo imefikia 800.

Vikosi vya usalama vikitumwa wakati wa maandamano Tunis, Tunisia.
Vikosi vya usalama vikitumwa wakati wa maandamano Tunis, Tunisia. REUTERS/Zoubeir Souissi
Matangazo ya kibiashara

Licha ya serikali kutangaza takwimu hizo, maelfu ya waandamanaji wamejitokeza leo Ijumaa kuendeleza maandamano dhidi ya serikali ya Tunis.

Waandamanaji hao wanalalamikia mpango wa serikali kuanzisha tena ubanaji wa matumizi ya fedha, suala ambalo wanasema linasababisha hali ya maisha kupanda.

Raia wa Tunisia wanasema bei ya bidhaa zimeanza kupanda, kinyume na ilivyokuwa hapo awali na shinikizo zinazoendelea ni kuitaka serikali kuachana na mpango huo.

Polisi wamekuwa wakitumia mabomu ya machozi kuwasambaratisha waandamanaji katika miji mbalimbali nchini humo, huku serikali ikiwashtumu waandamanaji hao kwa kupora mali ya watu.

Maandamano haya yameanza kuzua wasiwasi, kuwa hali inaweza ikawa kama mwaka 2011 wakati maandamano yalipomwondoa madarakani kiongozi wa wakati huo Zine El Abidine Ben Ali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.